02 August, 2015

Alikiba amesema tayari ameshafanya kolabo na msanii wa Congo DRC, Fally Ipupa Tazama video Hii

Mkali wa Bongo Fleva Alikiba amesema tayari ameshafanya kolabo na msanii wa Congo DRC, Fally Ipupa na kwamba ukifika wakati itatoka.
Alikiba ambaye yupo kwenye mikakati ya kufanya kolabo na Davido, ameiambia Clouds TV kuwa ikifika wakati ataiachia kolabo hiyo ambayo amedai ipo tayari. Tazama video hii akielezea jambo hiloMwana ilikuwa ni nyimbo ambayo nifanye na Fally Ipupa, beat imetengenezwa na Man Walter. Lakini kitu ambacho kilikwenda kutokea wakati nakwenda studio kufanya nyimbo nyingine kabisa, nikakuta Man Walter ameniandalia beat, ‘ile nyimbo yako unataka kufanya na Fally Ipupa hii hapa.’ Akaweka beat nikaanza ku-flow pale, nikaimbaimba nikapata melody. Kesho yake nikarudi nikafanya demo, kufanya demo nikarudi nyumbani nikakaa kama wiki, baada ya wiki moja nikaenda nikaimaliza yote,” alisema Kiba.

Lakini sasa tukakaa na Man Walter nikasema Fally Ipupa anaimbaje hapa? Akasema kwa kweli umeperfome vizuri sana, mimi naona ume-perfome vizuri sana. Tukapanga tufanye nyimbo nyingine. Basi akasema poa lakini Mwana ilikuwa Fally Ipupa aimbe. Kolabo na Fally Ipupa ipo, lakini kama ilivyo kawaida yangu napendaga kuwa-surprise watu kwa sababu watu wanakuwa hawajui Ali anafanya kitu gani muda wowote. Lakini ngoma ya Fally na mimi ipo na siwezi sema ni nyimbo gani lakini nyimbo ni nzuri sana na imesharekodiwa,” alisema Alikiba.

Pia Alikiba amesema kolabo yake na Davido ipo kwenye hatua nzuri na muda ukifika mashabiki wa muziki wake watajua lini itatoka.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...