Mchezo ulikuwa ni mkali na wa kasi, timu zote zilijitahidi
kutengeneza nafasi na kufanya mashambulizi kadhaa lakini milango yote
miwili ilikuwa migumu kuruhusu nyavu kutikiswa na washambuliaji wa timu
zote mbili.
Kombe hilo linawafanya Chile
wamalize ukame wa mataji nchini kwao hasa kwenye mchezo wa soka
kwasababu walikuwa hawajawahi kutwaa taji lolote kubwa la kimataifa.
Mchezaji nyota wa FC Barcelona
Lionel Messi, ameshindwa kutwaa taji kwa mara nyingine kwenye fainali
yake ya pili akiwa na Argentina baada ya mwaka jana (2014) kulikosa
kombe la dunia mbele ya Ujerumani kwenye fainali za kombe hilo
ilizofanyika nchini Brazil.
Messi ameshashinda mataji yote kwenye ngazi klabu, lakini ameshindwa kutwaa taji lolote akiwa ametinga uzi wa Argentina.
Matias Fernandez, Arturo Vidal, Charles Arangui na Alexis
walifunga mikwaju yao ya penati wakati wachezaji waliokosa penati kwa
upande wa Argentina ni Gonzalo Higuain ambaye alipaisha juu wakati
golikipa wa Chile Claudio Bravo alipangua mkwaju wa penati uliopigwa na
Ever Banega huku Messi akiwa ni mchezaji pekee aliyefunga penati ya
Argentina.
Matias Fernandez, Arturo Vidal, Charles Arangui na Alexis walifunga mikwaju yao ya penati wakati wachezaji waliokosa penati kwa upande wa Argentina ni Gonzalo Higuain ambaye alipaisha juu wakati golikipa wa Chile Claudio Bravo alipangua mkwaju wa penati uliopigwa na Ever Banega huku Messi akiwa ni mchezaji pekee aliyefunga penati ya Argentina.
NMEKUWEKEA VIDEO YA PENALTI ZOTE BONYEZA PLAY KUZITAZAMA>>>>>>>>>Usisumbuke Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,
No comments:
Post a Comment