07 July, 2015

Wakala wa Robin van Persie amekanusha taarifa zilizo zagaa kuwa Van Persie ameshakubaliana na klabu ya Fenerbahce

Van Persie 2Wakala wa Robin van Persie amekanusha taarifa zilizo zagaa kuwa Van Persie ameshakubaliana na klabu ya Fenerbahce lakini ameweka wazi kuwa, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uholanzi anarejea Carrington (uwanja wa mazoezi wa Man United) kujiunga na kikosi cha United kuanza mazoezi baada ya mapumziko ya mwishoni mwa ligi.
Inaeleweka kuwa, mpaka sasa hakuna dili lolote lililofanyika kati ya Manchester United na klabu hiyo ya Uturuki na vyanzo vya karibu kutoka kwa Van Persie vinasisitiza kwamba, mchezaji huyo anataka kuendelea kusalia Old Trafford kwa muda wote uliobakia kwenye mkataba wake.
 Van Persie 1Mshambuliaji huyo mwenye miaka 31 amepanga kukutana na kocha Louis van Gaal ili kufanya mazungumzo kujua nafasi yake kwenye kikosi hicho.
Alipoulizwa kwamba Van Prsie huenda akaondoka na anatafuta timu yenye uwezo wa kulipa pauini milioni 12 kufidia mkataba wake wa miezi 12 iliobaki kwenye mkataba wake, Kees Voss alisema: “Kama Robin angekuwa amepata timu mpya tu“Naweza sema kwamba Robin atajiunga na Manchester United kwa ajili ya mazoezi ya kwanza kwa ajili ya msimu ujao”.
Kilakitu kitategemea kama United watamsajili mshambuliaji mwingine, mshambuliaji wa Argentina na klabu ya Napoli Gonzalo Higuai na Edinson Cavan ambaye ni mkali mwingine wa timu ya taifa ya Uruguay na klabu ya PSG ndio miongoni mwa washambuliaji wanapewa nafasi kubwa ya kusajiliwa na Mashetani Wekundu.
Kama Van Persie atakuwa ni mshambuliaji chaguo la tatu, atalazimika kuikacha timu hiyo kwasababu nataka kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara kwenye kikosi cha kwanza ili aweze kupata nafasi ya kuitwa kwenye kikosi cha Uholanzi kitakachoshiriki michuano ya Euro mwaka 2016.
United tayari wako sokoni kutafuta mshambuliaji wa kuchukua nafasi iliyoachwa na Radamel Falcao na wanaweza wakamuuza Javier Hernandez ‘Chicharito’ na kumtoa kwa mkopo James Wilson.
ngeshaitangaza. Na kwasasa nipo Uholanzi”.

Usisumbuke Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...