Bondia
asiyepigika, Floyd Mayweather amevuliwa mkanda wa ubingwa wa WBO, uzito
wa Welterweight unaohusisha kilo 67 na 77 ambao alishinda mwezi Mei
mwaka huu dhidi ya Manny Pacquiao kutokana na kushindwa kufuata sheria
na kanuni za Shirikisho hilo.
Kamati
ya mashindano ya WBO imesema kwamba haina jinsi ya kufanya zaidi ya
kumvua mkanda huo Mayweather ambaye ameshindwa kulipa ada kutoka kwenye
pambano alilopigana na Pacquiao.
Ijumaa
iliyopita, ilikuwa siku ya mwisho kwa Mayweather kutimiza vigezo vya
ubingwa wa WBO ikiwemo kulipa ada ya dola laki mbili kutoka katika
pambano lake na Pacquiao pamoja na kujivua ubingwa wa uzito wa light-middleweight wa WBC na WBA.
Mayweather anayetajwa kuwa mwanamichezo tajiri zaidi Dunianiameshindwa kutelekeza agizo hilo, hivyo kamati imeamua kumvua mkanda wake wa kwanza wa WBO.
Bondia
Timoth Bradley Jr anatarajiwa kupewa mkanda huo baada ya mwezi uliopita
kumpiga kiutata, Jessie Vargas katika pambano la kutafuta bingwa wa
muda wa uzito huo, ingawa Mayweather mwenye umri wa miaka 38 amepewa
siku 14 za kukata rufaa.
Mayweather
bado anashikilia ubingwa wa welterweight na super-welterweight wa WBC
na WBA, ingawa kisheria, bondia haruhisiwi kushika ubingwa wa dunia
kwa madaraja mbalimbali.
Usisumbuke Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,
No comments:
Post a Comment