Jezi za Simba zimeanza kuuzwa
rasmi leo tarehe 30 – 7 – 2015 kwa mashabiki na wapenzi wa klabu ya hiyo
na wapenda mpira wa soka wote Tanzania.
Kama walivyoahidi
simbasports.co.tz imewapatia zawadi mashabiki wa Simba wawili wa kwanza
kununua jezi hizo, ambapo washindi ni Fabiani Mayenga na Amina Hussein.
Simbasports.co.tz ilifanya
mahojiano na mmoja wa washindi, Fabiani Mayenga na kusema “najisikia
vizuri sana kwa kuwa ndani ya klabu inayonijali sana, leo hapa nimekuja
kununua uzi mpya wa Simba na kupewa zawadi hakika nimefurahi sana na
ninaishukuru klabu yangu kwa kutujali wapenzi wake “.
Mayenga pia amewataka wapenzi
na mashabiki wa Simba kujitokeza mapema kununua jezi kwa TSH 15,000 ili
nao waweze kuichangia klabu yao kwani kununua jezi hizo na kuongeza
mapato kwa klabu tofauti na awali ambapo klabu ilikuwa haifaidiki na
jezi feki.
Kwa wakazi wa Dar es Salaam
wanaweza kupata jezi hizi makao makuu ya Simba pamoja na kwenye maduka
ya Uhl Sports yaliopo mtaa wa Sinza na Jamhuri, kwa wakazi wa mikoani
kwa sasa wanaweza kupata jezi hizi kupitia kwenye duka mtandao la Jumia
www.jumia.co.tz .
Simbasports.co.tz itaendelea
kutoa Jezi pamoja au tiketi ya VIP bure kwa wateja wawili wa kwanza
kwenda kushuhudia mechi zitakazochezwa siku ya Simba Day tarehe 8 – 8 –
2015.
No comments:
Post a Comment