Nyota aliyevunja rekodi ya usajili ya Manchester United, Angel Di Maria anaonekana kukaribia kujiunga na PSG.
Winga huyo wa Argentina mwenye
umri wa miaka 27 hakuwepo katika kikosi cha Man United kilichofanya
ziara ya maandalizi ya msimu mpya nchini Marekani, huku Louis van Gaal
akidai kwamba hajui lolote kuhusu alipo Di Maria.
Van Gaal alizungumza hayo na waandishi wa habari baada ya United kufungwa 2-0 na PSG alfajiri ya leo.
Mwandishi wa talkSPORT, Alan
Brazil ameleta kali baada ya ku-post tangazo huko Manchester akitangaza
kumtafuta Di Maria akitania kwamba amepotea.
Jamaa huyo amesema atakayemuona
Di Maria popote pale alipo ampigie simu Van Gaal kwa namba inayoonekana
pichani chini na atapewa zawadi ya paundi milioni 30.
No comments:
Post a Comment