29 July, 2015

Chege Chigunda amezungumza haya kuhusiana na kupost picha za mpenzi kwenye mitandao ya kijamii

Wapenzi wengi kwa sasa wanaamini juu ya suala la kuwekwa au ku post picha ya mpenzi wake kwenye account yake ya Instagram, Facebook au DP kwenye Whatsapp kuwa ndio kupendwa na kuamini kuwa hakuna mwingine zaidi yake.

Kwa msanii Chege Chigunda yeye alikuwa na mtazamo wake pale alio hojiwa na T-Bway 360 kwenye show ya 5Selekt kinacho rushwa na EATV kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 10 Jioni hadi saa 12 Jioni baada ya kuobwa achangie hoja 'Je kuna umuhimu wa ku post picha ya mpenzi wako kwenye mtandao wa kijamii?'.

Chege alisema kuweka au ku post picha ya mpenzi wako kwenye account yako sio kuonyesha mapenzi japokuwa inaweza kuongeza mapenzi. Kwake yeye amesema anweza hata ku post mara moja kwa mwaka au zaidi ila ni kutokana na vile atakavyo jisikia na sio kwamba ndio itaonyesha mapenzi yake ya dhati kwa mpenzi wake.

Chege Chigunda pia amezungumzia kuhusiana na shughuli zake za kimuziki kwa sasa na kuwataka Watanzania kuakaa tayari kwa ngoma zake mbili ambapo moja kaifanya na msanii wa Afrika Kusini na nyingine kaifanya na msanii wa Nigeria.

Chege ni moja wa wasanii ambao wametuza heshima yao kwa muda kwakuto sikika kwenye skendo mbaya nakusababisha heshima ya muziki wake kuzidi kusimama vyema.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...