Mahali pekee utakapopata habari za Burudani,Michezo,Urembo udaku na Kuelimika
05 July, 2015
USTAA WAMFANYA RUBY KUBADILI MPENZI (VIDEO)
Ruby star wa muziki ambaye ujio wake umekuwa ni wa kishindo kikubwa
katika tasnia ya muziki wa Bongo Flava, ametufungulia moyo wake na
kuweka wazi namna ambavyo safari yake katika usupa star imebadilisha
kabisa mahusiano yake ya kimapenzi. Kwa taarifa ambayo eNewz inakupa wewe kwa mara ya kwanza kabisa, The
Beautiful Ruby ambaye offcourse maisha yake yamebadilika na yanaendelea
kubadilika kwa kasi, amelazimika pia kubadili mahusiano yake ya
kimapenzi ambapo kwa sasa anatoka na mtu mpya na wanaelewana na kwenda
sawa bila kumuweka wazi hasa ni nani huyo.
Ruby ameeleza kuwa, mahusiano yake haya mapya yamemfunza kujishusha na
kuwa mfano bora kama kioo cha jamii, huku akifurahia zaidi umaarufu wake
kutia nakshi zaidi mahaba katika mahusiano hayo mapya.
Usisumbuke Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,
No comments:
Post a Comment