05 July, 2015

Muigizaji nyota mshindi wa tuzo la Oscar kutoka Kenya bi Lupita Nyon'go amesema kuwa anajivunia kuwa mwanamke mwenye nywele asili.


Lupita alisema kuwa licha ya kushamiri katika kilele cha anga za sanaa huko Holywood Lupita anasema anajivunia nywele zake asili.Lupita ambaye hunyoa nywele zake na wala hatumii dawa na kemikali za kunyosha nywele hizo anasema ''kama mwanamke mwafrika hana sababu ya kuaibikia muonekano wake asili''
''Nilihisi kama mtu aliyefunguliwa baada ya kukata nywele zangu zilizokuwa na kemikali ama ''perm''
Lupita alikuwa akizungumza na mwandishi wa BBC mjini Nairobi Kenya Anne Soy.
Bi Nyong'o aligonga vichwa vya habari aliposhinda tuzo la Oscar kufuatia mchango wake katika filamu ya ''12 years a Slave''.kwa sasa anaigiza katika filamu ya ''Americanah'' ambayo iliandikwa na msanii Chimamanda Ngozi Adichie kutoka Nigeria.
Mojawepo ya mada kuu katika riwaya hiyo ni siasa za nywele.
Kwa sasa bi Nyon'go aliyeteuliwa kuwa balozi wa maswala Mazingira wa shirika lisilokuwa la serikali la WildAid wildlife yuko nchini Kenya kuhamasisha umma kuhusu kazi hiyo yake mpya.

Usisumbuke Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...