Goli la Stars liliwekwa kambani
na John Bocco ‘Adebayor’ kwa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Uganda
kuunawa mpira akiwa kwenye eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo kuamuru
ipigwe penati, ndipo Adebayor alipoiandikia Stars goli hilo.
Lakini Uganda walisawazisha goli
hilo dakika chache baadae kupitia kwa Robert Sentongo baada ya mabeki wa
Stars kutegeana kuondosha mpira kwenye eneo lao la hatari na kufanya
matokeo kuwa 1-1.
Kipindi cha kwanza kilianza kwa
kasi huku Stars wakilishambulia kwa nguvu lango la Uganda ‘The Cranes’
ambapo dakika ya 18’ Simon Msuva alifunga goli lakini likakataliwa
kwasababu wakati anafunga goli hilo tayari alikuwa ameshaotea.
Simon Msuva, Deus Kaseke na
Rashid Mandawa walifanya kazi nzuri kipindi chote cha kwanza
wakigongeana pasi zilizowachanganya mabeki wa Uganda na kuifanya Stars
kuonekana kuwa na nguvu mpaya chini ya kocha Charles Boniface Mkwasa
aliyeichukua toka kwa Mart Nooij aliyetimuliwa baada ya Stars kufungwa
goli 3-0 na Uganda kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa
Amaan visiwani Zanzibar majuma mawili yaliyopita.
Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika timu zote zilikuwa hazijafungana licha mashambulizi kadhaa yaliyofanywa na timu zote mbili.
Kipindi cha pili kilianza kwa
kasi huku Stars wakiendelea kuliandama lango la Uganda kwa mashambulizi
makali ambayo hayakuwapa nafasi ya kupumzika walinzi wa timu ya Uganda.
Ramadhani Singano ‘Messi’
aliingia kuchukua nafasi ya Simon Msuva wakati Said Ndemla aliingia
kuchukua nafasi ya Frank Domayo na Rashid Mandawa akapumzishwa kumpisha
Salumu Telela.
Matokeo hayo yanaifanya Stars
kutupwa nje kwa jumla ya magoli 4-1 baada ya kupoteza mchezo wa kwanza
kwa goli 3-0 na leo kutoka sare ya kufungana goli 1-1 na kuwaacha Uganda
wakisonga mbele kwenye michuano hiyo ya CHANUsisumbuke Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,
No comments:
Post a Comment