Mshambuliaji inayeshinikiza kuondoka Liverpool, Raheem Sterling ametajwa kuwa ndiye mwenye
thamani kubwa kwa wachezaji vijana wenye umri chini ya miaka 21 barani
Ulaya, huku wanandinga wengine watatu wa England wakiingia kwenye orodha
ya 20 bora.
Kwa mujibu wa ripoti ya Soccerrex 20 U21,
Sterling amepewa thamani ya paundi milioni 35, ikiwa ni zaidi ya paundi
milioni 7 za Marquinhos wa PSG anayeshika nafasi ya pili.
Waingereza wengine ambao wameingia kwenye orodha hiyo ni mlinzi wa kati wa Everton, John Stones, mlinzi wa pembeni wa Manchester United, Luke Shaw na Calum Chambers wa Arsenal.
Hata
hivyo, kuna wachezaji wengine watano wa ligi kuu England katika orodha
hiyo, ingawa wawili kati yao hawajaanza kuzitumikia timu zao.
Nyota mpya wa Manchester United, Memphis Depay mwenye thamanin ya paundi milioni 23.5 ameshika nafasi
ya tatu, wakati mshambuliaji wa Liverpool, Divock Origi ambaye msimu
uliopita alicheza kwa mkopo klabu ya Lille ya Ufaransa ameshika namba 18
akiwa na thamani ya paundi milioni 10.7
Ripoti
ya Soccerrex 20 imezingatia vigezo mbalimbali ikiwemo kiwango cha klabu
katika ligi ya ndani na mashindano ya kimataifa, thamani ya mchezaji
kwenye soko la usajili pamoja na uwezo wa sasa wa timu yake kuuza
wachezaji kwa thamani kubwa.
No comments:
Post a Comment