Manchester United wameambiwa itawalazimu kulipa kiasi cha £13million na bonasi ya £1.4m ikiwa wanataka kupata saini ya beki wa kulia wa timu ya Torino, Matteo Darmian. ‘The Red Devils’ walituma ujumbe kwa Torino kuulizia namna ya kumsajili beki huyo ambaye anaichezea timu ya taifa ya Italia.
Rafael, amekuwa akiwindwa na vilabu vya Fiorentina, Galatasaray na Napoli – wakiungana na vilabu vingine viwili katika premier league ambao nao wanamtaka mbrazil huyo.
Darmian, ambaye ameshaichezea mara 13 timu yake ya taifa, ni miongoni mwa mabeki wa kulia ambao ni chaguo la kwanza la Louis Van Gaal.
Gregory Van der Wiel wa PSG, Seamus Coleman wa Everton na Fabinho wa Monaco – wao nao wamemvutia Van Gaal katika kutafuta mrithi wa Rafael.
Gazeti la kiitalianola Tuttosport limeripoti kwamba Manchester United wametuma ofa ya kwanza kwa ajili ya kumsaini Darmian, hata hivyo gazeti la Dailymail limeripoti kwamba vilabu vya United na Torino ndio vimeanza mazungumzo.
Usisumbuke Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,
No comments:
Post a Comment