Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
(VPL) itaanza Sept 12 badala ya Agosti 22 ili kumpa Charles Mkwasa fursa
ya kuendelea na program yake kuelekea mechi ya Taifa Stars dhidi ya
Nigeria itakayochezwa Sept 5.
Mechi ya Ngao ya Jamii (Community
Shield) itakayozikutanisha Azam FC dhidi ya Yanga SC sasa itachezwa
Agosti 22 badala ya Agosti 15.
Ratiba ya Ligi Kuu iliyokuwa
imeandaliwa, sasa inafanyiwa marekebisho kwa ajili ya tarehe mpya ya
kuanza, ambapo pamoja na mambo mengine mechi sasa zitachezwa wikiendi na
katikati ya wiki na wikiendi ya Oct 25 hakutakuwa na mechi kupisha
Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge.
Klabu za Ligi Kuu zimeandikiwa barua kujulishwa tarehe mpya ya kuanza Ligi, na dirisha la usajili linabaki kama lilivyo.
Wamiliki wa viwanja vyenye
upungufu wameandikiwa barua kutakiwa kurekebisha upungufu katika muda
maalumu, vinginevyo havitaruhusiwa kutumika kwa ajili ya PL na FDL.
Timu ya Madini ya Arusha
imeruhusiwa kutumia Uwanja wa Nyerere uliopo Mbulu mkoani Manyara kwa
mechi za SDL kwa masharti upungufu uliopo kwenye uwanja huo urekebishwe
kwanza.
No comments:
Post a Comment