21 July, 2015

Mapokezi ya Diamond toka kwenye ushindi wa MTV MAMA yamduwaza Yemi Alade

Mapokezi aliyoyapata Diamond Platnumz baada ya kurejea jana kutoka nchini Afrika Kusini alikoenda kuhudhuria tuzo za MTV MAMA, yalikuwa makubwa kiasi cha kumshangaza msanii wa Nigeria, Yemi Alade.
Diamond alishinda tuzo ya Best Live Act huku Yemi Alade akishinda ile ya Best Female Act aliyokuwa akishindana na Vanessa Mdee na wasanii wengine.

Yemi Alade ambaye ameshawahi kumshirikisha Diamond, amerepost kipande cha video kinachomuonesha Diamond akibebwa juu juu na mashabiki wake waliokuwa wakimsubiri kwa hamu kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julias Nyerere jijini Dar es Salaam na kuandika, “Kai chibu @diamondplatnumz the ultimate man! The love for you in Tanzania is not only ONLINE BUT VERY PHYSICAL !! WELLDONE BRO”

Yemi amedai kuwa ukubwa wa upendo anaopata Diamond sio wa mtandaoni peke yake bali hata katika mazingira ya kawaida.

Ushindi wa Diamond kwenye tuzo hizo umepokelewa kwa furaha kubwa na mashabiki wengi wa muziki nchini.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...