27 July, 2015

Mtoto wa Whitney Houston ‘Bobbi Kristina’ afariki dunia.

bobbi-kristina-brown
Mtoto wa Marehemu Whitney Houston na Bobby Brown ‘Bobbi Kristina’ amefariki dunia akiwa na miaka  22.
Bobbi amefia nje ya mji wa Atlanta kwenye nyumba ya uangalizi wa wagonjwa alipokuwa akiishi toka June 24 baada ya familia yao kuacha matibabu yote kutokana na ushauri wa daktari kuwa Bobbi hataweza kupona.
Kwa majonzi makubwa taarifa hii imethibitishwa na familia ya Bobbi Kristina na mazishi yameanza kupanga. Kwa upande mwingine polisi wameanza uchunguzi juu ya anayedai ni mume wa Bobbi ‘Nick Gordon’ akiwa miongoni mwa watu wanaohisiwa kutengeneza mazingira ya kumua Bobbi.
Bobby Brown amesema  “Sasa hivi tunachotaka ni kumzika binti yetu ili ampumzike kwa amani lakini upelelezi wa kifo chake utaanza rasmi baada ya mazishi haya, Mtu yeyote aliyehusika kusababishia kifo cha mwanangu lazima sheria ichukue mkondo wake”.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...