27 July, 2015

Msanii wa Afrika Kusini Donald adai Diamond ndio msanii mkubwa wa Afrika kwa sasa

Ukubwa wa Diamond Platnumz barani Afrika unazidi kuonekana wazi baada ya hivi karibuni kushinda tuzo za MTV MAMA na zile za African Achievers Awards zilizofanyika nchini Afrika Kusini.
Donald – msanii mkubwa wa nchini Afrika Kusini aliyemshirikisha Diamond kwenye wimbo wake, Wangu amedai kuwa muimbaji huyo wa Nana ndio msanii mkubwa zaidi Afrika kwa sasa.

“The biggest artist in Africa right now CONGRATULATIONS African Achievers Awards zilizotolewa Jumamosi hii jijini Johannesburg.

Kama hiyo haitoshi, wimbo wake Nana aliomshirikisha msanii wa Nigeria, Flavour umefikisha views zaidi ya milioni tatu ikiwa ni takriban miezi miwili tangu uwekwe. Msanii huyo pia anawania tuzo zingine kubwa barani Afrika (Nigeria na Uganda) na Marekani.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...