Winga wa Chelsea Eden Hazard ni
lazima azingatiwe kuwa miongini mwa wachezaji watatu bora wa dunia-
yaani juu ya Cristiano Ronaldo kwa sasa, hayo ni maneno ya kocha Jose
Mourinho .
Ronaldo na Lionel Messi
wamekuwa wakipokezana tuzo ya mchezaji bora wa dunia (Ballon d’Or), kwa
miaka ya hivi karibuni, huku wakiwa wanafunga mamia ya magoli huko ligi
kuu nchini Uhispania, lakini bosi huyo wa ‘The Blues’ amesema kitendo
cha Ronaldo kukosa kombe lolote msimu uliopita ndio sababu ya kuwa nyuma
ya Hazard.
Hazard alichukua tuzo ya
mchezaji bora wa ligi ya Uingereza msimu wa 2014-15 huku Chelsea
wakitwaa ndoo hiyo, hivyo Mourinho anasema hii ndio sababu ya winga wake
kupewa mazingatio makubwa katika hili.
“Ni dhahiri inategemeana na
msimu walionao”, aliwaambia waandishi. “Wanatakiwa kushinda makombe tu,
au sio? Mpira bila ya makombe ni sawa na hamna kitu”.
“Messi alishinda makombe
matatu. Ameshinda michuano mitatu mwaka jana, vile vile amefika fainali
ya Copa America. Alikuwa na msimu bora kabisa na kwa timu yake pia.
Sipendi wachezaji au mameneja wanajishindia tuzo binafsi bila ya timu.
“Msimu uliopita, ndio”,
Mourinho aliendelea wakati alipoulizwa kama Hazard alikuwa na msimu bora
kuliko Ronaldo”, bila kujali kwamba Ronaldo alikuwa yuko vizuri.
Alikuwa yuko vizurri sana. Alifunga idadi ya magoli ya kutosha tu.
“Sina shaka kwamba ni mchezaji
wa kiwango cha juu. Ninachosema ni kwamba, kwa mtazamo wangu, kila
mcheza soka duniani lazima aelewe kwamba timu lazima iwe mbele ya
makombe (timu kwanza, mchezaji baadaye)
“Eden anakuja kwa kasi sana
sasa na alipaswa kuwa moja ya wachezaji bora Ulaya mwaka uliopita.
Lakini kwa mtazamo wangu ni kwamba anatakiwa kuwa kwenye tatu bora na
sio kumi bora.
“Nadhani Eden ni mchezaji bora
wa nchi yetu. Mchezaji bora wa Uingereza. [Chama cha Waandishi wa Habari
za Soka] walimpigia kura pia, mchezaji bora wa EPL.Kama ilivyo ada EPL
ni ligi bora duniani, Nadhani ni miongoni mwa wachezaji wa kiwango cha
juu duniani”.
No comments:
Post a Comment