07 July, 2015

Mario Baloteli amekumbwa na matatizo ya kufiwa na baba yake wa kufikia ‘adaptive father’ wikend iliyopita.

balo
Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Italia, Mario Baloteli amekumbwa na matatizo ya kufiwa na baba yake wa kufikia ‘adaptive father’ wikend iliyopita. Baloteli mwenye asili ya Ghana alilelewa na mzazi huyo aliye mu-adapt tangu Mario akiwa na umri wa miaka 3 tu.
Wazazi hao waitaliano walio mlea mchezaji huyu waliishi nae huko kaskazini mwa Italia na kumlea kama mwanao wa damu. Tukio hilo la kupoteza mzazi wake limesababisha Baloteli akose kuhudhuria mazoezi ya klabu yake ya Liverpool katika hatua hizi za awali.
Liverpool walimuongezea likizo mshambuliaji huyo mkorofi ndani na nje ya uwanja ili apate utulivu zaidi katika kipindi hiki kigumu cha maombolezi.
Hata hivyo Liverpool wanaamini Baloteli atajiunga nao hivi karibuni ili waendelee na maandalizi yao ya msimu ujao wa 2015/16.
Wakati hup huo mchezaji Raheem Sterling wa klabu hiyo ya Liverpool ameendelea na mazoezi ya msimu mpya na klabu yake pamoja na kuwepo sintofahamu ya hatima yake.
Liverpool walikataa ofa mara mbili kutoka kwa Manchester City waliokuja na dau la pauni 40m za Uingereza lakini inaelezwa kuwa Liverpool wanamthaminisha mchezaji huyo kwa dau lisilopungua pauni 50m.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...