Timu Azam FC ‘Wanalambalamba’
wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya mihuano ya Kagame baada ya
kuitupa nje ya mashindano timu ya Yanga kwenye mchezo war obo fainali
uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa.
Timu hizo zililazimika kufika
hadi kwenye hatua ya mikwaju ya penati kufuatia kumalizika kwa mchezo
huku timu hizo zikiwa sare ya bila kufungana. Kwa mujibu wa kanuni za
mashindano ya Kagame,hatua ya robo fainali inapomalizika ndani ya dakika
90 bila imu kufungana zinakwenda moja kwa moja kwenye changamoto ya
mikwaju ya penati.
Aishi mManula alipangua penati ya
Haji Mwinyi ambayo ilikuwa ni penati ya tatu kwa upande wa Yanga na
kufanikiwa kuivusha timu yake hadi kwenye hatua ya nusu fainali ya
michuano hiyo.
Kipre Tchetche, John Bocco, Himid
Mao, Pascal Wawa na Agrey Morris walifunga mikwaju yao kwa upande wa
Azam wakati Salum Telela, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Godfrey Mwashiuya
walifunga penati zao huku Hajji Mwinyi yeye penati yake ikidakwa na
mlinda mlango wa Azam FC Aishi Manula.
Mpira ulianza kwa kasi sana
dakika za mwazo za kipindi cha kwanza, huku Azam wakifanya shambulizi
kali dakika hiyohiyo ya kwanza ambapo Kipre Tchethe alishindwa kufunga
goli baada ya….kupiga krosi iliyowapita walinzi wa Yanga na kumkuta yeye
ambae aliukosa mpira.
Azam hawakuishia hapo waliendelea
kufanya mashambulizi lakini wachezaji wa Azam hawakuwa makini kwani
hadi kipindi cha kwanza kinamalizika walikuwa wamekosa takribani nafasi
nne za kufunga.
Kwa upande wa Yanga, kipindi cha
kwanza hakikuwa kizuri sana kwao kwasababu hawakufanya mashambulizi
mengi ambayo yaliwashtua Azam. Shambulizi lililofanywa na Yanga
lilitokana na mpira wa kurusha ambapo Mbuyu Twite alirusha mpira
uliookolewa kwenye mwamba wa pembeni wa goli na mlinda mlango Aishi
Manula.
Wachezaji wa Azam walikuwa
wakitumia nguvu nyingi sana kuwakaba wachezaji wa Yanga hali ilyopelekea
mwamuzi kuwatuliza kwa kuwapa kadi za njano. Kheri Abdullah Salum,
Frank Domayo, Jean Mugiraneza na Ame Ally walioneshwa kadi za baada ya
kuwachezea vibaya wachezaji wa Yanga. Wakati kwa upande wa Yanga Juma
Abdul na Mbuyu Twite walioneshwa kadi za njano.
Kipindi cha pili kianza kwa Azam
kufanya mabadiliko kwa kumtoa Kreri Abdullah Salum na nafasi yake
ikachukuiwa na Said Morad wakati Frank Domayo ‘Chumvi’ alipumzishwa na
nafasi yake kuchukuliwa na Ame Ally ‘Zungu’. Yanga wao wakamuingiza
Salum Telela kuchukua nafasi ya Deus Kaseke wakati Juma Abdul alitoka
kumpisha Joseph Zutah na Malimi Busungu akaingia baada ya Amis Tambwe
kupumzishwa.
Kipindi cha pili bado Azam
waliendelea kukosa magoli kwani Kipre Tchetche, Ame Ally na Shah Farid
Mussa walikosa goli baada ya kujichanganya wao kwa wao na mpira kunyakwa
na mlinda mlango Ally Mustafa ‘Barthez’
Kwa matokeo hayo, Azam FC
inakamilisha timu nne zilizofuzu kucheza hatua ya nusufai naili ya
michuano ya Kagame kwa mwaka 2015 ambapo Ijumaa itakutana na KCCA ya
Uganda iliyofuzu kucheza hatua ya nusu fainali leo mchana kwa kuibanjua
timu ya Al Shandy ya Sudan kwa goli 3-0 huku Yanga wakiwa wameyapa mkono
wa kwaheri mashindano ya Kagame kwa mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment