Mtandao rasmi wa klabu ya Okwi umethibitisha kumsajili
MAELEZO MAFUPI YA TIMU MPYA YA OKWI
SønderjyskE ni shirika la michezo la Denmark linalomiliki timu ya mpira wa miguu inayoitwa SønderjyskE Fodbold, yenye makazi yake mjini Haderslev.
Pia linamiliki timu mbili za mpira wa mikono, SønderjyskE Håndbold, moja ya wanaume yenye masikani yake mjini Sønderborg, moja ya wanawake inayokaa mjini Aabenraa.
Pia lina timu ya ice hockey ijulikanayo kwa jina la SønderjyskE Ishockey, yenye makazi yake mjini Vojens.
Timu zote hizi zinacheza ligi za kaskazini mwa Jutland inayojulikana kwa jina la Sønderjysk Elitesport (Kwa kiingereza: Southern Jutlandic Elite Sport).
SønderjyskE ni timu iliyoundwa kwa ajili ya Jimbo zima la Jutland kaskazini kwa lengo la kuleta ushindani katika ligi za juu za Denmark na timu hii iliweka maskani yake mjini Haderslev ikiitwa Haderslev FK.
Mwaka 2004, timu zote, yaani ya mpira wa miguu, ice hockey na handball chini ya Shirika hilo la SønderjyskE, zilianza kuwakilisha ukanda mzima wa Jutland Kaskazini na sio mji mmoja tena. Zilivuta hisia za watu, wadhamini, mashabiki na vyombo vya habari kutokana na kuchukua vijana wengi wenye vipaji .
Kwasasa timu 5 zinacheza katika ligi bora za Denmark, huku timu ya mpira wa miguu ikiwa tishio katika ligi kuu ya Denmark.
Hizi ndizo timu zinazoshiriki ligi kuu ya Denmark kwa msimu wa 2015/2016
Matokeo ya mechi za karibuni za timu ya Okwi na ratiba ijayo…
No comments:
Post a Comment