10 July, 2015

Hatimaye klabu ya Liverpool ya Uingereza imemtangaza kiungo wake Jordan Henderson, kuwa nahodha mpya wa klabu hiyo

vvvvvvvvvvv
Hatimaye klabu ya Liverpool ya Uingereza imemtangaza kiungo wake Jordan Henderson, kuwa nahodha mpya wa klabu hiyo yenye maskani yake Merseyside. Henderson ambaye alikua nahodha msaidizi wa ‘Captain Fantastic’ Steven Gerrard msimu uliopita alitarajiwa kuchukua nafasi hiyo mara baada ya Steven Gerrard kutangaza kuihama klabu hiyo ambapo amejiunga na LA Galaxy ya MLS Marekani.
Ujio wa mchezaji James Milner katika kikosi hicho msimu huu kulitia shaka nafasi ya Henderson kumrithi Gerrard kutokana na uzoefu wa Milner mwenye miaka 29.
Hata hivyo wakiwa katika maandalizi ya msimu mpya, kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers ameona ni muhimu kumtangaza Henderson ambaye amekua ni moja ya nguzo muhimu katika kikosi cha Liverpool.
Henderson ambaye alijiunga na Liverpool akitokea Sunderland alikaribia kuondoka kikosini hapo misimu mitatu iliyopita ili ampishe Clint Dempsey wa Fulham wakati huo.
Hata hivyo nahodha huyo mpya wa Liverpool, alikataa kuondoka kikosini hapo huku akiomba apewe nafasi, aoneshe uwezo wake.
Unahodha huo wa Liverpool umekuja wakati muhimu, wakati ambao Steven Gerrard amekaririwa hivi karibuni akimpigia chapuo Henderson kurithi mikoba yake.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...