United wanahitaji mchezaji ambaye
anaweza akacheza kama mlinzi wa kulia baada ya kocha wa kikosi hicho
Louis van Gaal kusema kwamba, mbrazil Rafae ameshindwa kuimudu nafasi
hiyo.
Ieleweke kwamba, Man United
imekuwa kwenye mazungumzo na Darmian, 25, na wanamatumaini ya kufikia
makubaliano ya kumsajili nyota huyo kwa kiasi cha pauni milioni 11.
Darmian ni mchezaji wa kimataifa
wa Italia ambaye ameshaitumikia timu yake ya taifa kwa michezo 13 na
michezo sita akicheza muda wote (full time), Van Gaal anaamini mchezaji
huyo atamsaidia kwenye nafasi ya ulinzi wa kulia.
Pia
Van Gaal anatarajia kumuachia Rafael aondoke kabla ya kuanza kwa msimu
mpya lakini atasikiliza ofa pia juu ya mlinzi wa kati John Evans ambaye
mpaka sasa bado hajapewa mkataba mpya.
Usisumbuke Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,
No comments:
Post a Comment