31 July, 2015

Hii ndio taarifa kamili ya BASATA kuhusu kumfungia shilole mwaka mmoja kutojihusisha na kazi za sanaa


Balaza la sanaa Tanzania (BASATA) limetangaza kumfungia mwanamziki wa Kike shilole kutojihusisha na kazi za sanaa kwa mwaka mmoja ndani na nje ya nchi.  Adhabu hii imetolewa kufuatia shilole kupigwa picha za aibu wakati akitumbuiza nchini ubeligij mname tarehe 09/05/2015 .
“Tarehe 9 May 2015 ukiwa katika onyesho lako la muziki Ubelgiji ulicheza uchi mbele ya hadhira ya wapenda sanaa za Tanzania hivyo kudhalilisha utu wako na jamii ya kitanzania kimaadili
BASATA ilipata habari zako, kumbuka pia October 2013 BASATA lilikuonya na ukakiri kwa kuomba msamaha tabia yako ya kucheza bila kuzingatia maadili uwapo jukwaani, BASATA ilikupa nafasi ya kutoa maelezo kwanini usichukuliwe hatua za kinidhamu kwa kitendo chako lakini umekaidi kutoa maelezo yako
Baraza limejiridhisha kwamba ulikiuka maadili ya kazi ya sanaa kwenye onyesho lako huko Ubelgiji makusudi na umekiuka sheria kwenye ibara ya 30 (2) ya katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 kwa kuvunja maadili ya jamii ya Mtanzania hivyo baraza linakusimamisha kujishughulisha na kazi za sanaa nchini na nje ya nchi kwa mwaka mmoja, kufanya kinyume na hayo kutapelekea kupewa adhabu zaidi pamoja na yeyote utakaeshirikiana nae”
Hii ndio barua yao

Hii ni moja ya picha zilizomponza shilole Shilole 2

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...