31 July, 2015

Ben Pol kufanya collabo na Jason Derulo kutoka Marekani

Mfalme wa R&B Tanzania, Benard Michael Paul a.k.a Ben Pol ameweka wazi mipango yake ya kuupeleka muziki wake kimataifa kwa kutafuta collabo na wasanii wakubwa wa kimataifa.

Ben Pol ambaye kwa sasa yuko nchini Kenya alikoenda kushiriki kwenye msimu mpya wa kipindi cha Coke Studio Africa, amesema kuwa miongoni mwa wasanii ambao anategemea kufanya nao collabo ni pamoja na hit maker wa “Wiggle”, Jason Derulo kutoka Marekani.

Hit maker wa “Sophia” ameweka wazi mpango huo alipokuwa katika session ya kuulizwa maswali na mashabiki kupitia ukurasa wa Facebook wa Coca Cola.

Shabiki alimuuliza Ben pol endapo akipata nafasi ya kuchangua msanii wa kufanya naye collabo wa kimataifa atamchagua nani?

“Kwa sasa nafikiria kufanya collabo na Jason Derulo, kwa sababu ni msanii mchapakazi na anayezidi kukua na kuvuka mipaka siku hadi siku, Menejimenti yangu inaendelea kumtafuta, natumai tutafanikiwa.” alijibu Ben Pol.

Hadi sasa Ben Pol tayari amefanya collabo na Nameless na Rabbit wa Kenya.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...