Theo Walcott amekubali kusaini mkataba mpya na klabu yake ya Arsenal.
Nyota huyo wa Uingereza (26), alikuwa anaingia katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake na ‘The Gunners’.
Lakini baada ya mazungumzo ya muda mrefu kati yake na viongozi wakuu wa klabu ya Arsenal, dili hilo sasa lianenda kukamilika.
Dili hilo litambakisha Walcott
klabuni hapo mpaka mwaka 2019 na kumfanya alipwe kiasi cha mshahara wa
pauni 100,000 kwa wiki na kuwa moja ya wachezaji wa Arsenal wanaolipwa
pesa ndefu zaidi.
Arsenal watathibitisha rasmi
makubaliaono hayo wiki mbili zijazo, pengine kabla ya kuanza kwa msimu
mpya wa EPL, ambapo watafungua dimba wakiwa nyumbani Emirates na klabu
ya West Ham.
Olivier Giroud:yupo katika wakati mgumu baada ya Walcot kuonesha njaa na nafasi yake ya mshambuliaji wa kati.
No comments:
Post a Comment