Baada ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa
Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete kulianga rasmi bunge mjini Dodoma
msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz ameguswa na
hotuba hiyo.
Diamond Platnumz ameamplify leo kwenye AMPLIFAYA na kusema’Kipindi
ambacho nimebahatika kumuona Mheshimiwa madaraka na vitu ambacho
amevifanya kiukweli ni vitu ambavyo vinagusa sana hususa katika tasnia
ya kwetu ya muziki unajua hatujawahi kupata mheshimiwa ambaye akawa
anatizama suala la muziki na kulithamini kama la kwake kabisa sio tu
suala la muziki na vitu vingi sana mimi sio mtu wa kusikiliza masuala ya
siasa wala kuangalia masuala ya kisiasa‘ – Diamond Platnumz
‘Leo kwa Mara ya kwanza nilikuwa naendesha gari huku nasikiliza vitu
mwanzo mpaka mwisho kuna vitu ambacho alikuwa anazungumza vinagusa
moyoni kabisa kuna vitu alikuwa anaongea vya kuchekesha lakini kuna time
nilikuwa nafikiri Je rais atakaekuja atakuaje atakuwa kweli anakumbuka
jamii yake ukizungumzia kama wasanii na watu wengine kama alivyokuwa
anafanya yeye kwasababu sio kila mtu anachukulia suala la sanaa kama
serious mwingine anaweza akaona vijana hawa wanaimba imba tu lakini
wengine ndio ajira yetu tunafamilia wazazi wetu ndugu marafiki na
tumeajiriana wenye wenye’ – Diamond Platnumz‘Nikajikuta ghafla daah Je Rais atakayekuja ikiwa Je anapenda uvuvi akiwa anapenda vitu vingine labda muziki akaudharua itabidi tukashika nyavu tukavue na suala la muziki linaishia hapo hapo hakuna masuala ya Channel O au MTV nikajikuta nawaza nikajikuta naandika kutoka moyoni hakika katutoa kule anatuacha hapa ambako pako juu zaidi kama kauli yake mwenye alivyosema inagusa moyoni yaani unatamani kama inawezekana wala apewa muhula mwingine aendele tena lakini ndio haiwezekani kisheria lakini ndo hivyo namshukuru sana nampongeza kwa kipindi ambacho akiwa akilihutubia taifa la Tanzania’ – Diamond Platnumz
No comments:
Post a Comment