11 July, 2015

Bastian Schwesteiger athibitishwa kwenda Man United – awek rekodi hii

Klabu ya Manchester United imekubaliana kimsingi na mabingwa wa Bayern Munich juu ya usajili wa kiungo wa timu ya taifa ya Ujerumani Bastian Schweinsteiger.
  Bastian, mwenye umri wa miaka 30, aliomba mwenyewe klabu ya Bayern Munich kutompa mkataba mpya na angependa kwenda sehemu nyingine.
Mkurugenzi mkuu wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge ameongea na waandishi wa habari muda mfupi uliopita na kusema: “Marafiki zangu wa pale Manchester United tumekuwa na mawasiliano kwa muda kidogo. Tumefikia makubaliano juu ya uhamisho wa Bastian.
Schweinsteiger ameshaichezea Bayern Munich mechi 536 tangu alipovaa jezi ya timu hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2002.
 
Inamaanika kwamba Bastian amevutiwa kujiunga na Manchester United kutokana na kuwa na mahusiano mazuri na kocha Louis van Gaal ambaye alimfundisha soka wakati alipokuwa kocha wa Bayern Munich.
Ada ya uhamisho iliyolipwa kumsajili Schwesteiger inaaminika kuwa karibia kiasi cha £8m na mshahara wake utakuwa kiasi cha £7m kwa mwaka.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...