Mayweather ambaye ameshinda
mapambano 48 aliyopanda ulingoni bila sare wala kupoteza akishinda
mapambano 26 kwa ‘knockout’, anashikilia mataji ya WBC na WBA katika
uzito wa ‘welter’ aliudhihirishia ulimwengu ubora wake kwa kumtwanga kwa
wingi wa alama mpinzani wake Many Pacquiao katika pambao lililovunja
rekodi ya mapato katika mchezo wa ngumi ulimwenguni.
Mmarekani huyo aliyepokonywa
mkanda wa WBO baada ya kukiuka masharti mapema wiki hii, ametuma ujumbe
kwenye mtandao wa kijamii ukiashiria kurudi kwake ulingoni kabla ya
kuisha kwa mwaka huu.
“Kwa mashabiki wangu. Uaminifu
wenu na sapoti yenu vimenipa miaka 20 bora ambayo ningeiomba. Na nikiwa
juu, napanga kwenda juu. Tukutane tena ulingoni Septemba 12,” ulisomeka
ujumbe wa Mayweather.
Taarifa hizo zinaweza kuibua
fununu nyingi juu ya nani atavaana na bondia huyo katika pambano hilo
kwani mabondia kadhaa wameshatajwa kupanda naye ulingoni akiwemo Andre
Berto aliyeshinda mapambano 30 na 23 kwa ‘knockout’ pamoja na Karim
Mayfield aliyeshinda mapambano 19 huku 11 kati ya hayo akimaliza kwa
‘knockout.’
Mwingine anayevumishwa kupanda
ulingoni na bingwa huyo ni bingwa wa zamani wa dunia Amir Khan ambaye
kwa kipindi kirefu amekuwa akisaka nafasi ya kuzichapa na Mayweather
bila mafanikio lakini itawabidi wapenzi wa ndondi kusubiri mpaka
itakapotangzwa rasmi ni bondia gani atakwenda kuendeleza au kuvunja
rekodi ya nguli huyo wa mchezo wa masumbwi ulimwenguni kwa sasa.
No comments:
Post a Comment