Mashine ya BVR zalipua moto mkoani Arusha, chama cha CHADEMA mkoa wa Arusha leo kufanya maandamano makubwa kupinga hujuma katika uandikishaji wananchi katika daftari la kudumu.
Kuna stori nyingine imesikika leo kutoka mkoani Mara ambako mtoto wa miaka 12 Penina Joseph ageuka bubu baada ya kung’atwa na mamba mwaka jana akiwa mtoni anachota maji.
Stori nyingine inatoka nchini Kenya ambako Gavana wa Benki kuu ya Kenya Patrick Ngoroje mwenye umri wa miaka 54 azua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kusema kua hajaoa mpaka sasa licha ya umri kumtupa mkono, Gavana huyo aliibuka kidedea baada ya kuchaguliwa na rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kua Gavana wa Benki Kuu ya nchi hio mwaka huu.
Hapa chini iko sauti ya stori zote hizi bonyeza play kuzisikiliza.
No comments:
Post a Comment