Serikali ya Tanzania inatarajia kukopa kiasi cha dola milioni mia nane
za Kimarekani kutoka taasisi mbili za kifedha za kigeni ili kuimarisha
shilingi ya Tanzania ambayo inaendelea kudorora.
Tayari Tanzania imefanya mazungumzo na
taasisi hizo mbili ,Rand Merchant
Bank ya Afrika Kusini pamoja na Benki ya Maendeleo ya China.Benki kuu ina matumaini kwamba fedha hizo ambazo serikali ina mpango wa
kukopa kwa ajili ya bajeti yake zitasaidia kuimarisha shilingi.
Katika kipindi cha miezi sita tu, tayari shilingi ya Tanzania imeshuka
kwa asilimia 21 na kuwa kati ya sarafu inayofanya vibaya zaidi barani
Afrika.
Mkurugenzi wa utafiti wa uchumi na sera Dr Joseph Masawe ameiambia BBC
kwamba hata kama lengo kuu la ukopaji wa fedha hizo halikuwa kuimarisha
shilingi, upatikanaji wake katika mzunguko wa fedha utasaidia
kuiimarisha shilinigi.
"Swala la kukopa pesa nje si geni. Karibu kila mwaka serikali hukopa
pesa nje na nia kubwa si kuimarisha shilingi lakini ni kwa ajili ya
kutekeleza bajeti yake" amesema Dr Masawe
Dr Masawe amesema sababu za mporomoko ya shilingi ni lazima ziangaliwe
kwa mapana na kwamba sababu nyingine zipo nje ya uwezo wa taasisi yake
na serikali ya Tanzania.
Amezitaja baadhi ya sababu hizo kuwa ni pamoja na kuimarika kwa uchumi
wa Marekani ambapo umechangia karibu asilimia 65 ya mporomoko huo wakati
sababu zingine ni kama vile uchaguzi ujao na uingizwaji wa bidhaa
nyingi kutoka nje mambo ambayo hayaepukiki
Wiki iliyopita Waziri wa Fedha wa Tanzania Saada Mkuya aliliambia bunge
kuwa serikali ina mpango wa kupunguza utegemezi katika bajeti yake
kutoka kwa nchi wahisani kwa asilimia 6.4 katika mwaka huu wa fedha.
Hata hivyo mkakati huo umetiliwa shaka na wachambuzi wanahofu kwamba
unaweza kuongeza deni la taifa ambalo hadi mwezi wanne mwaka huu
lilifikia takribani dola bilioni 18.9
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7
KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...
-
C9 Records presents STAR by Foby!. Click DOWNLOAD button bellow to download this song.
-
John ana mke ambaye haoni uzuri wa kitu chochote anachofanya, akifika tu nyumbani mke wake huanza kumlalamika kuwa hela anayoacha nyumba...
-
Mboga za majani na matunda zimekuwa zikisisitizwa kwa sana na wataalamu wa afya hasa kwa wanawake wajawaziti kwani zimekuwa zikiongeza Damu...
No comments:
Post a Comment