19 June, 2015

Ambwene Yesayah 'AY' awashauri Diamond na Alikiba wafanya kazi pamoja

Rapper Ambwene Yesayah maarufu kama AY ametoa ushauri kwa Diamond na Alikiba kuweka tofauti zao pembeni na kufanya muziki pamoja.AY ametoa ushauri huo baada ya kuulizwa na shabiki kupitia Kikaangoni cha EATV aliyetaka kujua ni msanii yupi kati ya wawili hao anayemkubali zaidi.


“Wote wawili ni wasanii wazuri na nawashauri wafanye kazi pamoja siku si nyingi,” alijibu AY.

Rapper huyo pia amewashauri mashabiki kutowachonganisha wasanii hao ambao wamekuwa na uadui wa miaka mingi.
“Upendo ndio suala la msingi,tusichonganishe watu tuweke bidii watu wafanye kazi pamoja,” aliongeza.

Hivi karibuni uhasama kati ya wasanii hao wawili wanaopendwa nchini uliongezeka zaidi hasa baada ya kumalizika kwa tuzo za KTMA ambapo walikuwa wakishindana kwenye vipengele vingi.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...