Klabu ya Manchester United
imetangaza rasmi kukamilisha usajili wa nyota wa kimataifa wa Uholanzi,
Memphis Depay na kumsainisha mkataba wa miaka minne.
Mpango wa kumsajili kinda huyu
mwenye miaka 21 ulikamilika mwezi uliopita, lakini sasa dili
limekamilika rasmi ambapo United imelipa ada ya uhamisho ya paundi
milioni 25.
Kiungo huyo anajiunga na
Manchester United kutokea klabu ya PSV Einhoven ambapo alionesha kiwango
cha juu kwenye ligi ya Uholanzi akifunga magoli 22 msimu uliopita.
Kijana huyo pia ameonesha
kiwango kizuri timu ya taifa na wiki iliyopita alicheza mpira mwingi mno
Uholanzi ikifungwa 4-3 na Marekani.
Memphis Depay anakuwa mchezaji
wa kwanza kusajiliwa rasmi na Man United majira haya ya kiangazi ambapo
Louis van Gaal anatafuta wachezaji wa kuimarisha kikosi cha kushindania
ubingwa msimu ujao.
No comments:
Post a Comment