NIPASHE
Serikali imesema kuwa inafanya utaratibu wa kuwalipa fedha takribani Sh. bilioni 19 za waliokuwa wanachama wa Taasisi ya Development Entrepreneurship Community Initiative (Deci).
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, alisema fedha hizo zimehifadhiwa katika akaunti ya Benki Kuu (BoT) na kwamba kinachofanyika sasa ni uangalizi wa kiasi cha michango iliyochangwa na
wanachama ili waweze kulipwa kwa usahihi.
“Bado
fedha zinashikiliwa BoT uchambuzi unaendelea kufanywa kwa umakini wa
hali ya juu, utakapokamilika wanachama wote waliochanga fedha
watalipwa,” Mkuya.
Aidha, Waziri Mkuya alisema siyo jambo
litakaloweza kuchukua muda mfupi kukamilisha mchakato wa malipo ya
wanachama hao, kwani linahitaji muda wa kutosha kufanyiwa kazi
kikamilifu, ingawa hakutaja kiasi kilichopo.
Mwaka 2009 serikali ilisitisha shughuli
za Deci na kuwafungulia mashtaka wakurugenzi watano wa taasisi hiyo
katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam na Agosti
19, mwaka 2013, walihukumiwa.
NIPASHE
Wabunge wamefichua ufisadi katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC,
mkoani Kilimanjaro, ambayo watendaji wakuu wa hospitali hiyo wameuziana
magari mapya ya serikali kwa bei ya kutupa ya Sh. milioni 8 kila moja.
Ubadhirifu huo ni wa kutisha uliibuliwa
jana Bungeni wakati mjadala wa hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Afya na
Ustawi wa Jamii kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016.
Mbunge wa Viti Maaalum Chadema, Suzan Lyimo,
alisema viongozi wakuu KCMC wameuziana magari aina ya Prado na Nissani
Patro kwa bei ya Sh. milioni 8 kila moja mwaka 2013, ambayo yalipelekwa
katika hospitali hiyo kwa shughuli mbalimbali.
Alisema kutokana na ubadhirifu huo Mhasibu wa hospitali hiyo, Paulo Muhunya, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Afya (TUGHE), alimjulisha Rais Jakaya Kikwete, kwa kumtumia ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kuhusu ufisadi huo.
Lyimo alisema katika hali ya kushangaza
Mhasibu huyo baada ya kutoa taarifa za ubadhirifu huo, Mei 5, mwaka huu,
alisimamishwa kazi jambo ambalo linatia mashaka.
“Nchi
hii inashangaza inakuweje mtu aliyesaidia kutoa taarifa za kufichua wizi
yeye ndiye anaadhibiwa, au ndio utaratibu wa serikali ya CCM kuwalinda
wezi,” .
Naye Mbunge wa Viti Maalum Chadema, Congesta Lwamlaza, alisema Serikali ya CCM ni ya kutumbua tu ndiyo maana fedha nyingi zinatengwa kwa mambo ya starehe tu.
NIPASHE
Chama Cha Wapangaji Tanzania, kimeiomba
Wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kutokubali kuuza nyumba za
Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),
zilizopo katikati ya miji hasa Upanga jijini Dar es Salaam, kwa kuwa
wanaotaka kuzinunua ni matajiri wachache wenye kiu ya kunufaika na
rasilimali za nchi.
Aidha, chama hicho kimeishauri serikali
kusitisha upangaji wa muda mrefu kwa nyumba za NHC, ili Watanzania wengi
hasa wanaoanza kazi waweze kunufaika na nyumba hizo.
Katibu Mkuu wa chama hicho, Ndumey Mukama,
alisema utafiti wao umebaini kuwa kuna wapangaji wa kudumu NHC ambao
sasa wanataka kuuziwa nyumba hizo kwa bei ya kutupa wakati tayari
wameshajenga nyumba maeneo mengine.
Alisema wapangaji wa muda mrefu wa NHC
hasa maeneo ya mjini kama Dar es Salaam ni watu wenye uwezo ambao
wengine wamejenga nyumba nzuri na wanazipangisha kwa dola za Marekani,
huku wakiendelea kulipa kodi ndogo NHC.
Alisema wapo wanasiasa wachache na baadhi ya wapangaji wa muda mrefu wanaong’ang’ania kuuziwa nyumba hizo kinyume cha utaratibu.
Aliishauri Serikali iweke sheria ya
ukomo wa upangaji wa nyumba za serikali angalau miaka mitano ili kutoa
nafasi kwa Watanzania wengi hasa wanaoanza maisha kuweza kupanga nyumba
hizo.
Mukama alisema:
“Utaratibu wa sasa wa wapangaji kukaa kwa muda mrefu katika nyumba hizo
umewajengea kiburi wapangaji hawa na wamefikia hatua ya kutaka kuuziwa
nyumba hizi kwa bei chee wakati ni rasilimali ya Watanzania wote. Hawa
wanaouwezo wa kununua nyumba zinazojengwa sasa katika maeneo mengine na
NHC wakanunue huko.”
Alisema jambo lingine linalowapa kiburi
wapangaji wa NHC ni kusikilizwa ‘sana’ na serikali hata pale ambapo
wanakiuka masharti ya upangaji.
Chama hicho pia kimeishauri serikali
itengeneze sera ya nyumba ambayo itawabana pia wenye nyumba binafsi na
kuweka usawa kwenye sekta hiyo.
MWANANCHI
Tofauti na makada wengine Magufuli, jana alichukua fomu kimyakimya bila kutaka kuzungumza lolote.
Badala yake akasema atatafuta muda
muafaka wa kuzuwa CCM ambao walianza kwa kutangaza nia kisha baada ya
kuchukua fomu kuzungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Ujenzi, Dk
John ngumza na vyombo vya habari baada ya kusoma fomu alizopewa na chama
chake.
Hata hivyo, kwa kifupi kabisa alisema
endapo atapata ridhaa ya kuiongoza nchi atatekeleza Ilani ya CCM na
kuwaomba Watanzania wamuombee.
Dk Magufuli ambaye alikuwa amevalia
suruali nyeusi na shati la kijani, hakuwa na mbwembwe za wapambe wengi
kama ilivyokuwa kwa wagombea wengine.
Alisindikizwa na watu watatu akiwamo, Mbunge wa Nkenge, Assumpter Mshama na wapambe wawili walioshuka katika gari lake.
Kada huyo alichukua fomu yake saa 11.30 jioni na kisha kuondoka zake katika eneo hilo kimyakimya.
MWANANCHI
Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja
ametangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, huku akiahidi kupambana na
mambo sita aliyoyaita maadui wakuu wa nchi ambayo ni umaskini, ujinga,
maradhi, rushwa, ufisadi na mmomonyoko wa maadili.
Akitangaza nia hiyo kwenye Ukumbi wa
Benki Kuu ya Tanzania (BoT) Mwanza jana, Ngeleja alisema anatambua
kwamba Watanzania wa leo wanatamani kumpata rais ambaye atapambana kwa
dhati na vitendo na maadui hao.
“Nina
mikakati madhubuti ya kujibu swali la kiutafiti linaloonyesha kwamba
mamlaka, idara na taasisi za umma zenye dhamana kubwa ya maisha ya
Watanzania mfano, Polisi, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mahakama,
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na watendaji wakuu
wa taasisi za biashara (CEO) ndiyo wanaoongoza kwa tuhuma za kupokea
rushwa,”.
Ngeleja akiwa ameambatana na mkewe, Blandina na Mwenyekiti wa Kamati yake ya Maandalizi, Mbunge wa Magu, Dk Festus Limbu
waliingia ukumbini saa sita mchana na kupokewa na makada wa CCM
waliohudhuria ambao walitoka maeneo mbalimbali ikiwamo vyuo vikuu,
wajumbe wa halmashauri kuu kutoka bara na visiwani, wawakilishi wa
wamachinga na wavuvi.
Alisema Watanzania wanatamani kuwa na
rais ambaye atasimamia kwa dhati umoja na mshikamano wa kitaifa,
Muungano, kulinda amani, kukemea kwa nguvu zote ubaguzi wa dini, kabila,
rangi na aina nyingine yoyote ya ubaguzi inayoweza kujitokeza nchini na
kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama wa mipaka ya nchi.
“Historia ya nchi yetu ni ndefu na imepita misukosuko mingi lakini kwa umoja, udugu na mshikamano wetu tumefanikiwa,” .
Hata hivyo alisema hivi sasa rushwa, ufisadi, uvivu na mmomonyoko wa maadili ni maadui wengine walioongezeka kwa kasi.
“Kadri
Watanzania tunavyozidi kuongezeka kwa idadi na maadui zetu hawa nao
wanazidi kujitanua. Hivyo mbinu, mikakati na silaha za kupambana na
maadui hawa lazima zibadilike,” alisema.
Ngeleja alisema baada ya kushauriwa na
baadhi ya Watanzania kutoka pande zote za nchi tena wa kada mbalimbali
amejitafakari, kujitathmini na kujiridhisha kuwa anayo dhamira ya kweli
kuwatumikia Watanzania.
“Nimejitafakari,
nimejitathmini na kujiridhisha kwamba ninayo dhamira ya kweli ya
kuwatumikia Watanzania kupitia nafasi ya urais. Mbali ya dhamira ya
kweli nimejipima kwamba ninao uwezo wa kubeba matarajio ya Watanzania,
kupitia utekelezaji wa kaulimbiu yangu isemayo: “Maono Sahihi, Mikakati
Thabiti, Matokeo Halisi (MMM),” alisema.
MTANZANIA
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa,
amechukua rasmi fomu ya kuomba kuteuliwa kuwania urais kupitia Chama
Cha Mapinduzi (CCM), huku akisema hana mpango wa kushindwa.
Lowassa aliwasili katika Makao Makuu ya CCM mjini hapa jana saa 10:20 jioni akiambatana na mkewe, Regina huku akisindikizwa na wabunge mbalimbali pamoja na wanachama wa CCM.
Lowassa alisema hawezi kuzungumzia upande wa kushindwa katika safari yake.
“Swali rahisi sana, sina mpango wa kushindwa,” alisema Lowassa alipokuwa akijibu swali aliloulizwa na waandishi wa habari kama atashindwa katika kinyang’anyoro hicho.
Alipoulizwa kuhusu hali ya nchi kuwa na
watu wanaoshambuliwa, Lowassa alisema atajenga Serikali itakayojali utu
na uhuru wa vyombo vya habari.
“Kwanza
nimpe pole yule mwandishi wa MTANZANIA aliyeteswa. Sikubaliani na mambo
ya kuingilia uhuru wa watu kuteswa. Serikali yangu itaheshimu uhuru wa
vyombo vya habari,” alisema Lowassa huku akishangiliwa na wanachama wa CCM waliokuwa wamefurika ndani na nje ya ukumbi huo.
Alipoulizwa kwanini anahusishwa na
vitendo vya ufisadi, Lowassa aliyekuwa akijibu maswali kwa ufupi,
alisema kama kuna mtu ana ushahidi na tuhuma hizo amtaje jina.
“Kama
hawakunitaja hawakunihusisha… Mtu anayejiamini aseme, na anitaje.
Nachoka na siasa za tuhuma, hatupimi viongozi kwa rekodi za matusi ila
tutawapima kwa matendo yao,” alisema.
Kada huyo wa CCM alivitaka vyombo vya
habari kutoshabikia tuhuma zisizo na ushahidi, huku akisisitiza kuwa
kila mtu apimwe kwa rekodi yake.
Kuhusu uteuzi wa mawaziri, Lowassa hakutaka kulizungumzia akisema bado hajavuka daraja.
Kuhusu Serikali ya Umoja wa Kitaifa,
alisema ni sera ya CCM iliyotekelezwa baada ya kutokea mgogoro kati ya
vyama vya CCM na CUF.
“Angalieni
kule Marekani, vyama vya Democrat na Republican, vinashindana kwa kura
chache sana. Hata sisi tunapishana kwa kura chache, mimi nadhani kama
hatupishani sana hivyo hilo ndilo suluhisho,”.
Naelewa
matatizo wanayopata watumishi wa CCM, nayaelewa. Mishahara midogo,
hawakopesheki, hawana fedha za likizo na hawana uchumi mzuri. Wakati
wengine wanajengewa nyumba na mikopo wenyewe hawapati,” Lowassa.
Hata hivyo, alimsifu Rais Jakaya Kikwete kwa kuimarisha uchumi ndani ya chama hicho, lakini akasema akiwa rais atafanya zaidi.
“Tunaweza kufanya zaidi, tusiwe
ombaomba. Nilipokuwa mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini tumejenga jengo
la ghorofa 22 Dar es Salaam. Tuna viwanja na maeneo mengi. Nikichaguliwa
kuwa rais na mwenyekiti nitaangalia hilo…Bila CCM madhubuti nchi yetu
itayumba,” .
MTANZANIA
Upelelezi wa kesi inayomkabili Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Mchungaji Josephat Gwajima na wenzake watatu umekamilika na kesi inatarajiwa kuanza usikilizwaji wa awali Julai 2, mwaka huu.
Wakili wa Serikali Mwandamizi, Shadrack Kimaro aliifahamisha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana wakati kesi hiyo ilipokuwa inatajwa.
Mbele ya Hakimu Mkazi Hellen Riwa,
Kimaro alidai kesi ilikuwa inatajwa, lakini upelelezi wa kesi hiyo
umekamilika hivyo aliomba tarehe nyingine ya kuwasomea washtakiwa
maelezo ya awali.
Hakimu Riwa aliyakubali maombi ya upande wa Jamhuri na kuahirisha kesi hadi Julai 2, mwaka huu.
Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni msaidizi wa askofu huyo, Yekonia Bihagaze, mfanyabiashara George Mzava na mkazi wa Kimara Baruti, Geofrey Milulu .
Katika kesi ya kwanza namba 85, Gwajima
anadaiwa kati ya Machi 16 na 25, mwaka huu katika Viwanja vya Tanganyika
Packers Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam alitoa lugha ya matusi dhidi
ya Askofu wa Kanisa Katoliki, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo kwamba ni mtoto, mpuuzi asiye na akili katika namna ya kwamba ingeleta uvunjifu wa amani.
Katika kesi ya pili namba 84, Gwajima
anakabiliwa na shtaka moja la kushindwa kuhifadhi silaha na risasi
kinyume cha sheria ya uhifadhi wa silaha za moto.
Anadaiwa kwamba kati ya Machi 27 na 29,
mwaka huu ndani ya Jiji na Mkoa wa Dar es Salaam, alishindwa kuhifadhi
silaha aina ya Beretta namba CAT 5802 , risasi tatu za pisto na risasi
17 za shotgun.
HABARILEO
Baraza Kuu la uongozi la Chama cha Wananchi (CUF)
limemchagua kwa kura zote 56 Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif
Hamad kuwa mgombea wa nafasi ya urais wa Zanzibar kwa tiketi ya chama
hicho katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa chama hicho, Omar Ali Shehe
alisema maalim amepita bila ya mpinzani katika kinyang’anyiro cha
nafasi ya urais wa Zanzibar kutokana na imani kubwa ya wanachama wa
chama hicho dhidi yake.
Alisema uamuzi huo sasa utamfanya Maalim
Seif kumsubiri mgombea kutoka katika Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa
ajili ya kinyang’anyiro cha nafasi hiyo.
“Chama
cha CUF kimebadilisha utaratibu zamani jina la mgombea wa nafasi ya
urais linaamuliwa na mkutano mkuu wa chama, lakini tumebadilisha maamuzi
hayo kutokana na gharama kubwa za kuitisha mkutano katika chama
kichanga kama hiki,” alisema.
Mapema Shehe alitangaza majina ya mwisho
ya wagombea wa nafasi ya Uwakilishi na Ubunge katika chama cha CUF
katika majimbo 50 ya Unguja na Pemba.
Katika majina hayo yanaonesha kwamba Mbunge wa Mkanyageni, Mohamed Habib Mnyaa ambaye aliangushwa katika kura za maoni amerudishwa kuwania nafasi hiyo katika jimbo hilo.
Aidha, Mbunge wa jimbo la Mji Mkongwe kwa tiketi ya CUF, Mohamed Ibrahim Sanya
ameondolewa katika kinyang’anyiro hicho na nafasi yake kuchukuliwa na
mwandishi mkongwe aliyekuwa akifanya kazi katika Shirika la Utangazaji
la Uingereza (BBC), Ali Saleh.
Sanya aliibuka nafasi ya kwanza katika
mchakato wa kura za maoni huku akimuangusha vibaya kwa kupata kura 21
Ali Saleh ambaye alishika nafasi ya tatu.
Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi
alipoulizwa kuhusu maamuzi ya Baraza la Kuu la Uongozi wa CUF, alisema
baadhi ya vigezo muhimu vilipewa kipaumbele cha kwanza ikiwemo suala
zima la matokeo ya kura za maoni kutoka katika majimbo ya uchaguzi kwa
wanachama.
Aidha, alisema suala la utekelezaji na
kukubalika katika jamii ni suala la pili ambalo lilizingatiwa kwa lengo
la kuona mgombea anafanikiwa na kukivusha chama hadi kupata ushindi.
“Vipo
vigezo tulivipa kipaumbele cha kwanza ikiwemo matokeo ya awali ya kura
za maoni za wanachama katika majimbo ya uchaguzi, lakini pia suala zima
la utekelezaji na kukubalika katika jamii,” alisema.
JAMBOLEO
Jeshi la Polisi linamshikilia mkazi wa Mabibo, Salma Said
kwa kosa la kujaribu kuiba mtoto katika hospitali ya Mwananyamala
jijini Dar es salaam huku akidai amefanya hivyo ili kulinda ndoa yake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es salaam Camillius Wambura alisema mtuhumiwa alikamatwa na polisi baada ya kupata taarifa kutoka kwa uongozi wa hospitrali hiyo.
Wambura alisema mtuhumiwa alifika
hospitalini hapo na kuwadanganya wenzake kuwa amejifungua mtoto njiti
huku akionekana kujificha wakati wauguxi wakipita kuangalia wagonjwa
mbalimbali katika wodi ya wazazi.
“Mtuhumiwa
alikamatwa na muuguzi wa zamu wakati akijaribu kuiba mtoto katika wodi
ya wazazi, alikamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria” alisema Mganga mkuu wa hospitali hiyo.
Mtuhumiwa huyo alidai kuwa ameamua
kufanya hivyo ili kulinda ndoa yake, na hadi sasa ana watoto wawili
ambao kila mmoja ana baba yake na wanahudumiwa na mwanaume anayeishi
naye kwa sasa, hivyo alifanya hivyo ili kudumisha ndoa yake zaidi.
Hata hivyo mama mkwe wa mtuhumiwa
alikana na kudai hamtambui na kudai si mke halali wa mtoto wake licha ya
familia yake ma familia hiyo ilikana kumtolea dhamana mtuhumiwa huyo
No comments:
Post a Comment