hadi sasa angekuwa amefika mbali zaidi ya hapo alipo, hasa katika kujitangaza kimataifa ikiwa ni pamoja na kufanya collabo na wasanii wa nje.
Barnaba amezungumza na Bongo 5 na kutoa sababu za kwanini hadi sasa hajaanza kuonesha jitihada za kwenda kimataifa.
“Watu wengi wanaamini kwamba Barnaba ana package ambayo inajitosheleza kwenda International, na mimi mwenyewe naamini kuwa nina package ya kutosha ukizingatia watu wanavyoni include, Barnaba mwandishi, composer, muimbaji, Barnaba ana studio yake. Ofcourse kweli ni maamuzi na kuna kujipanga, Sio kama siumii na sio kama sipendelei, ofcoz hata mimi mwenyewe nahitaji kuwa International lakini International mwenye package ya kujitosheleza.” alisema Barnaba.
Ameongeza kuwa anatamani kuwa kama wasanii wakubwa wa Afrika lakini kutokana na malengo yake ya kutaka kuliteka kwanza vizuri soko la nyumbani ndio maana mpaka sasa bado hajaweka nguvu nyingi kwenda kimataifa.
“Mi natamani kuwa kama kina Sauti Sol, natamani kuwa kama Kina Maurice Kirya, kina Youssou n’dour, kina Lokua Kanza, kina P-Square, 2 Face, natamani kuwa lakini sio kwamba siwezi naweza lakini nafikiri mkakati wangu unaenda taratibu taratibu, package yangu ilikuwa kwanza kushawishi nyumbani wanielewe kwenye package ambayo inajitosheleza, naamini nyumbani wamenielewa lakini kuna kiasi ambacho sijatosheka nacho.”
“Safari ya kwenda International iko tayari na imeanza lakini hakuna kitu kizuri kama kufanya ukaonesha watu kuliko kuzungumza kwa watu, niko kwenye kufanya niwaoneshe watu nitakapokuwa tayari kuwaonesha wataona. Kwa sasa hivi nafanya album yangu ambayo itavuka International ukizingatia video, kuna wasanii ambao nimewashirikisha wengi ni International mule ndani, mimi huwa ni kobe ambaye naenda taratibu taratibu na nafikiri taratibu taratibu yangu huwa inaleta makubwa sana.” alimaliza.
No comments:
Post a Comment