Ame (kushoto) baada ya kusaini Azam fc
AZAM FC leo imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Mtibwa Sugar, Ame Ally ‘Zungu’ na kumsainisha mkataba wa miaka miwili.
Makamu mwenyekiti wa Azam fc,
Nassor Idrissa ‘Father’ amethibitisha kuinasa saini ya Ame na kusema
wameshamalizana na klabu ya Mtibwa.
Idrissa ameongeza kuwa Straika
huyo aliwavutia kwa kiwango chake cha juu msimu wa 2014/2015 akiwa na
Wakata miwa wa Manungu na wanaamini chini ya kocha mkuu Stewart Hall
anaweza kuisaidia Azam kuliko alivyoisaidia Mtibwa Sugar.
No comments:
Post a Comment