UGANDA ‘The Cranes’ imeitandika
2-0 Botswana katika mechi ya ufunguzi ya kundi D kuwania kufuzu kombe
la mataifa ya Afrika (Afcon 2017) iliyopigwa leo uwanja wa Nelson
Mandela, Namboole, mjini Kampala.
Magoli ya Uganda yamefungwa na
Geoffrey Massa dakika ya 55′ na Mshambuliaji wa zamani wa Azam fc, Brian
Umony katika dakika ya 66′.
Uganda waliingia kwenye mechi
hii wakipewa nafasi kubwa ya kushinda kutokana na rekodi nzuri ya hivi
karibuni hususani mechi za kufuzu.
Kabla ya mechi ya leo Uganda walikuwa wemeshinda mechi 7 kati ya 7 walizocheza za kufuzu katika uwanja wa nyumbani.
No comments:
Post a Comment