Moja ya story kubwa kwenye siasa za TZ
wiki iliyopita ilikuwa ishu ya CCM kuwafungulia makada wake sita ambao
walikiuka kanuni za chama hicho kwa kutangaza kugombea Urais mapema
kinyume na utaratibu wa chama hicho, mmoja ya waliokuwa wamefungiwa ni
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Ngoyai Lowassa.
Jana kulikuwa na stori ya Naibu Waziri Mwigulu Nchemba kutangaza kugombea Urais wa TZ kupitia CCM.. leo Mbunge Edward Lowassa
ameongea kuhusu mambo kadhaa ikiwemo hali ya afya yake, chuki kwenye
siasa, na ujumbe wake kwa CCM kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 TZ.
Ishu ya chuki kwenye siasa >>”Kuna
chuki imeibuka kwenye siasa za nchi yetu na kutakiana mabaya, afya ni
neema kutoka kwa Mungu.. mimi niko sawa kabisa kwa chochote kile..
kwenye Chama chetu waweke utaratibu tukapimwe wote afya mimi nitakuwa wa
kwanza kwenda kupima tuelezane nani mgonjwa“>> Edward Lowassa.
Sentensi yake nyingine kuhusu tatizo la ajira>>>”Tatizo
la ajira ni bomu lisiposhughulikiwa.. toka nimetoka Serikalini kuna
vitu ambavyo kama tungevifanya kwa kasi ile ambayo tulianza nayo
ningepita napunga mkono nikapata kura zote, hatufanyi maamuzi iwe magumu
au rahisi.. mambo yanakwenda legelege, Rais amefanya jitihada kubwa
sana lakini kuna mambo hayaendi>>> Edward Lowassa.
Suala la elimu>>>”Tukiwekeza vizuri katika elimu tunaweza kubadilisha nchi yetu.. Tukitaka kuokoa nchi yetu tuwekeze kwenye elimu“>>> Edward Lowassa.
Kuhama CCM je? >>>”Kuhama
chama sina mpango.. nimeingia CCM toka 1977 sijafanya kazi mahali
pengine popote isipokuwa CCM.. My life is CCM.. huyo ambae hanitaki CCM
ndio ahame sio mimi nihame“>>> Edward Lowassa.
Kauli yake kuhusu visasi >>> “Mimi ni Mkristo, ninaamini kwenye dini yangu sana… sina kisasi na mtu yoyote“>>>
“Upinzani
umeanza kupata nguvu kubwa sisi ni chama dola tusibweteke.. wenzetu
wanajiandaa vizuri na sisi tujiandae vizuri. Tusifanye mchezo
tusibweteke”>>> Mbunge Edward Lowassa.
Kwa dakika tatu kayazungumza haya, sauti yake unaweza kuisikiliza hapa kwa kubonyeza play !!
No comments:
Post a Comment