Kesho Jumatano saa kumi jioni
katika tasnia ya Kabumbu nchini wapenda soka macho na masikio yao
yatakuwa katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam kushuhudia Mtanange
wa Mabingwa wapya wa VPL Yanga SC pamoja na Mabingwa waliokuwa watetezi
Azam FC huku
kukiwa na dua mbalimbali za timu nyingine zikiombea neema upande mmoja na Kuomba zahama kwa upande wa pili.
kukiwa na dua mbalimbali za timu nyingine zikiombea neema upande mmoja na Kuomba zahama kwa upande wa pili.
Bila shaka katika Mtanange huo
Simba watakuwa wakiishangilia Yanga ili iweze kushinda dhidi ya Azam ili
waweze kujiwea pazuri katika kuwania nafasi ya pili ambayo pia Azam
wanaitaka kwa udi na ubani, Azam wao watakuwa wakiomba ili waweze
kushinda na kujihakikishia ushiriki wa michuano ya kimataifa hapo
mwakani.
Kuelekea mtanange huo
Shaffihdauda.com imezungumza na viongozi wa timu zote mbili, Katibu mkuu
wa Yanga Dk Jonas Tiboloha pamoja na Meneja wa Azam FC Jemedali Said
ambapo kila mmoja amesema mchezo huo wanauchukulia kama fainali kwani ni
muhimu kwao, Yanga ikitaka kukabidhiwa kombe lao kwa heshima ya
kutofungwa na aliyekuwa bingwa mtetezi, Huku Azam wakitaka kushinda ili
wapate nafasi ya ushiriki wa michuano ya kimataifa Afrika hapo mwakani.
Jemedali Said amesema kuwa baada
ya kufungwa na Simba waliendelea na mipango ya timuwachezaji wakiwa
kambini kwa kutambua umuhimu wa Mchezo.
“Ndio Tunaelekea mchezo na Yanga
na maandalizi yetu yako vizuri kama ambavyo tumekuwa tukifanya siku zote
kwasababu hata kabla hatujacheza na Simba tulikwisha amua kwamba timu
itakaa kambini hadi hapo ligi itakapokuwa imekwisha, Baada ya kupoteza
na Simba siku ya Jimapili timu imerejea ambini na jana imefanya mazoezi
jioni na leo itafanya mazoezi jioni tayari kwa mchezo wa kesho, Kwahiyo
sisi kama Timu tumejiandaa tunajua ni moja kati ya mechi ngumu kabisa,
Hatujawahi kucheza na Yanga alafu mechi ikawa nyepesi siku zote mechi
inakuwa ngumu”
“Muda huu ugumu unaongezeka
kwasababu tayari Yanga wamekwisha kabidhiwa ubingwa sisi kesho tutakacho
kifanya ni kwaajiri ya mabingwa kama itakavyokuwa, Tunaamini kuwa
matokeo yake yakiwa mazuri kwetu itakuwa ni faida kwasababu tutakuwa
tumepata nafasi ya kwenda kushiriki michuano ya kimataifa kwa mara nne
mfurulizo, Lakini tunajua ugumu uliopo wa kupata matokeo hayo ambayo
sisi tunayategemea” Amesema Jemedali Said Meneja wa klabu ya Azam FC.
Kwa upande wa Yanga ambao tayari
kulikuwa na uvumi kuwa watachezesha wachezaji wa kikosi cha pili na
kuwapumzisha nyota wao kwasababu tayari wamekuwa mabingwa,Dr. Tiboloha
amekanusha vumi hizo kwa kusema watapambana mwanzo mwisho ili kuondoa
aibu ya kufungwa na bingwa mtetezi.
“Labda nikuhakikishie tu kitu
kimoja cha siri kwamba, Nilisema wiki mbili zilizopita nilipokuwa
nikilalamikia ratiba ya ligi na ninaendelea kusema tena leo, Yanga
hatuta pumzika, tutapumzika Ligi ikimalizika baada ya mchezo wa Ndanda
FC, Kwamaana hiyo sisi tutaingiza kikosi chetu kamili kesho kwa maana
hiyo kila mchezaji ambaye yupo fit atacheza, Na nimechi ambayo sisi
tumedhamilia kushinda kwasababu haitaleta maana yoyote kwa watu tumesha
kuwa mabingwa alafu twende tukafungwe na mtu aliyekuwa bingwa tetezi
ambaye tumemnyanganya ubingwa,”
“ Kwa maana hiyo tunaingia tukiwa
tumedhamilia kushinda na tunajua mechi ni ngumu na tunaingia tukiwa
tunawaheshimu kama tulivyokuwa tunawaheshimu timu nyingine zilizopita,
Tunajua Azam ni timu ambayo imeundwa vizuri, inawachezaji wazuri,
inacheza mpira mzuri achilia matokeo ambayo walikuwa wanayapata hivi
karibuni lakini sisi tukiangali wanaupande mzuri sana kwahiyo ni mechi
ambayo hatuta legea kwa kitu chochote kile na kwa namna yoyote ile,
kwahiyo tunaenda kucheza tukijua ni lazima tuondoke tukiwa tumeshinda
mchezo huo” Amesema Katibu huyo wa Yanga Dr. Tiboloha.
Kwa upande wa Jemedali Said
Meneja wa Azam FC alipotakiwa kuelezea changamoto zilizopelekea kufanya
vibaya kwa msimu huu ikiwa hata katika michuano ya klabu Bingwa
kuondolewa mapema alijibu kama ifuatavyo.
“Ni kweli kwamba ukiangalia msimu
huu ulivyokuwa ukilinganisha na timu ilivyokuwa msimu uliopita ni
dhahiri kwamba hatujafanya vizuri, Hatujafanya vizuri kwa maana kwamba,
kwanza hatujafika mbali kwenye mashindano ya kimataifa Champions league
tumetolewa raundi ya mwanzo, Marengo yeu ya pili ilikuwa kutetea Ubingwa
kwahilo tumefail pia maana Yanga wamechukua, Lakini kwakuwa msimu
haujaisha leo niseme wapi tumejikwaa na nini kimesababisha nadhani
itakuwa bado mapema mno sisi bado tunamichezo miwili”
“Utaratibu ambao sisi tumejiwekea
ni kwamba kuna sehemu kama tatu ambazo zinatoa ripoti ya msimu mzima
ulivyokuwa , Benchi la Ufundi kupitia kwa mwalimu mkuu aliopo sasa
George Nsimbe Best ataleta ripoti yake, mimi pia kama meneja nina Ripoti
yangu pia Utawara kwahiyo zote zikisha jumlishwa ndio tunajua nini kwa
msimu mzima tunarekebisha, Kwahiyo mwisho wa msimu ndio nitatoa jibu la
mapungufu yalikuwa yapi” Amesema Jemedali Said.imu hizo mbili kesho zitakutana katika Uwanja wa Taifa Jijini
Dar es salaam kucheza mchezo wao ambao ni kipolo, lakini tukio kubwa
baada ya kumalizika kwa mchezo huo Bodi ya ligi pamoja na Wadhamini wa
ligi ambao ni Vodacom watawakabidhi Yanga kombe lao la Ubingwa ambao
wameuchukua Msimu huu wa 2014/15 wakiwapokonya Azam FC waliouchukua
mwaka jana.
No comments:
Post a Comment