05 May, 2015

Utajiri wa Dangote kaamua kuwekeza na kwenye michezo?? Macho yake yanaitazama Arsenal!!

emiiMwaka 2010 Aliko Dangote ambaye ni tajiri namba moja Afrika kutokea Nigeria aliahidi kununua hisa kutoka klabu ya Arsenal, lakini ikashindikana na sasa amerudi tena.
Dangote ambaye ni mfanyabiashara maarufu amesema kwa sasa ameweka nia ya
kuitaka klabu hiyo aimiliki na tayari ameanza mazungumzo.
Bilionea huyo mwenye utajiri wa zaidi ya dola bilioni 15 ni tajiri mara nane ya alivyokuwa wakati alipojaribu kununua hisa za klabu hiyo kwa mara ya kwanza na kwamba bado hajatupilia mbali ndoto yake ya kutaka kuinunua klabu hiyo iliyopo Kaskazini mwa Landon.dangoteee
Amesema matumaini yake ni makubwa na atainunua kwa bei ambayo wamiliki wake hawataweza kukataa.
Arsenal ni moja ya timu kubwa zinazofanya vizuri katika ligi kuu ya England na kwa sasa iko katika nafasi ya tatu kweye ligi kuu ya nchini humo.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...