Mabingwa wapya wa ligi kuu ya
Soka Tanzania bara, Klabu ya Dar es salaam Young Africans inatarajia
kukabidhiwa kikombe chake cha ubingwa siku ya jumatano baada ya mchezo
dhidi ya Azam FC katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kaimu Mtendaji mkuu wa Bodi ya
Ligi Tanzania, Fatma Abdullah amesema kuwa wameamua kuipatia Yanga
kikombe cha Ubingwa siku hiyo ikiwa ni kabla ya mchezo mmoja ili
kumalizika kwa ligi hiyo kufatia kuwa mchezo wa mwisho watakuwa ugenini
Mtwara huku Jumatano watakuwa wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani.
“Tumewasiliana na Wadhamini
Vodacom hivyo Siku hiyo Yanga tutawakabidhi kombe lao, Tumefanya hivyo
kwasababu watakuwa katika Uwanja wao wa Nyumbani kama unavyojua mchezo
wa mwisho watakuwa Mtwara” Amesema Fatma Abdullah.
Yanga wamefanikiwa kuibuka
Bingwa wa VPL kwa msimu wa 2014/2015 baada ya kufikisha pointi 55 ambazo
haziwezi kufikiwa na timu yoyote katika ligi huku wakiwa na michezo
miwili mkonono ukiwemo huo wa jumatano dhidi ya Azam FC ambao ndio
walikuwa mabingwa watetezi huku hadi sasa wakiwa hawana uhakika wa
kupata hata nafasi ya pili ambayo inawaniwa pia na Simba SC.
No comments:
Post a Comment