16 May, 2015

WENGER HANA BUDI KUSHABIKIA BARCELONA #UEFA KWA SABABU HIZI


Usiku wa jumamosi ya tarehe 6, June 2015, macho na masikio ya wapenzi wa soka ulimwenguni kote yataelekezwa jijini Berlin, Ujerumani katika dimba la OlympioStadio ambapo FC Barcelona itacheza dhidi ya Juventus katika fainali ya UEFA Champions League.

Maelfu ya mashabiki wa vilabu hivyo viwili watasafiri kuelekea huko Berlin lakini FC Barcelona itakuwa na shabiki mmoja wa kipekee – kocha wa timu ya Arsenal – Arsene Wenger.
Endapo FC Barcelona watashinda mechi hiyo na kutwaa ubingwa wa tano wa ulaya, basi Arsene Wenger ataungana na mamilioni ya mashabiki wa Barca kushabikia ubingwa huo – huku Wenger akiiwakilisha klabu yake atakuwa akienda benki akicheka maana kutokana na ushindi huo, Arsenal watalipwa kiasi cha £3million na Barca.Arsenal watalipwa fedha hizo kutokana na makubaliano waliyoingia na Barca wakati wanawauzia beki Thomas Vermalain mwanzoni mwa msimu huu. Gunners walipokea kiasi cha £15million kutoka Barca na Wenger aliweka kipengele cha Barca kuwaongeza bonasi ya £3m ikiwa klabu hiyo ingetwaa ubingwa wa ulaya.
Kutokana na kiwango hicho cha fedha, Wenger ana sababu ‘millioni 3′ kuiombea Barca ishinde.

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...