MWANANCHI
Wakati Mkutano wa Bunge ukianza kwa
mjadala wa uliopoteza mwelekeo na kutawaliwa na malumbano kati ya
Wabunge wa CCM na wa Vyama vya Upinzani, Naibu Spika Job Ndugai amesema ni vigumu hali hiyo kuzuilika kwa kuwa mwaka huu ni mwaka wa Uchaguzi. Bunge hilo
lilipokea na kuanza kujadili Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo yaliibuka malumbano ya kisiasa huku Wabunge wa Upinzani wakilalamikia udhaifu wa Serikali katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa miaka 10 iliyopita.
lilipokea na kuanza kujadili Hotuba ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo yaliibuka malumbano ya kisiasa huku Wabunge wa Upinzani wakilalamikia udhaifu wa Serikali katika utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwa miaka 10 iliyopita.
“Mwaka huu
ni wa Uchaguzi huwezi kuzuia hiyo hali na kumbuka kuwa Wabunge ni
Wanasiasa.. Wabunge homa zipo juu na hawawezi kukaa hapa wakati katika
Majimbo yao wanapigiwa simu kuwa yamevamiwa”—Naibu Spika Job Ndugai.
Baadhi ya Wabunge walisema agenda kuu
kwa sasa ni Uchaguzi Mkuu kwa kuwa hiki ni kikao cha mwisho cha Bunge na
baada ya hapo wote wanarudi Majimboni kwa ajili ya Uchaguzi.
MWANANCHI
Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe
imewabana walimu wa Shule ya Sekondari ya Msimbu na kuwataka waandike
barua kujieleza baada ya kushika nafasi ya mwisho Kiwilaya katika
matokeo ya Kidato cha Pili na kidato cha nne 2014.
Mkurugenzi wa Wilaya hiyo, Mwamvua Mrindoko alisema waliunda Kamati kuchunguza sababu ya kufeli huko.
Mrindoko amesema
baadhi ya sababu walizobaini kuchangia kufeli kwa wanafunzi wengi iko ya
ushirikiano duni kati ya shule na Jamii, msukumo mdogo wa wazazi kwenye
elimu pamoja na utoro wa wanafunzi.
NIPASHE
Kutokana na machafuko yanayoendelea
Burundi na kusababisha kufurika kwa waomba hifadhi mkoa wa Kigoma, kambi
ya Nyarugusu imejaa na kusababisha shule zilizopo ndani ya kambi hiyo
kufungwa kwa muda.
“Kwa
kawaida kambi hii ina uwezo wa watu 50,000 kulingana na taratibu za
kimataifa, lakini mpaka sasa ina wakimbizi 54,706…hivyo baada ya kuanza
kuwapokea waomba hifadhi wapya Aprili 29, mwaka huu, tumepata wapya
16,808 hadi juzi”– alisema Mkuu wa kambi hiyo, Sospeter Boyo.
Alisema kwa sasa wamefunga shule ili
majengo hayo yatumike kuwahifadhi wahamiaji wapya wanaowasili kila siku
huku wakifanya jitihada kupata sehemu nyingine ya kuwahifadhi.
Baadhi ya wakimbizi kambini hapo, walisema kitendo cha kushindwa kuondolewa madarakani kwa Rais Pierre Nkurunzinza, kimewasikitisha kwani kitasababisha kuwapo na machafuko zaidi.
“Tunasikitika
sana kwa jaribio hilo kutofanikiwa, sasa hali itakuwa mbaya zaidi
nchini kwetu kutokana na machafuko ya kushindwa kuondolewa madarakani
Nkurunzinza”– alisema mmoja wa wakimbizi hao.
Wakimbizi hao wamesema Demokrasia ndani
ya Burundi imepotea na pia kunafanyika mauaji ya kimya kimya kwa
wananchi wenye mlengo tofauti na Rais aliyepo madarakani.
NIPASHE
Mbunge Suleiman Said Bungara ‘Bwege’ ametofautiana
na wabunge wenzake wa upinzani wanaosema Serikali ya CCM imechoka,
badala yake amesema Watanzania ndio waliochoka huku akisema kuwa wapo
wabunge wanaoitetea serikali kwa kuibeba, lakini wapo wabunge wanaofanya
kazi zao za kuikosoa.
Bwege alisema serikali haijachoka kama
wengine wanavyosema isipokuwa waliochoka ni Watanzania wanaoibeba
serikali hiyo wamechoka, wamejiandaa kuiondoa madarakani katika uchaguzi
mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu na kuwaweka wagombea wa
UKAWA madarakani.
“Fungeni
virago muondoke… anakuja Mbunge hapa na kusema serikali imejenga shule,
Zahanati halafu baadaye wanaomba/wanalalamika miradi ya maendeleo katika
majimbo yao haijatekelezwa.. Wabunge wa CCM wamechoka, wanajiaga
wenyewe”—Suleiman Bwege.
Hoja ya kuchoka kwa Serikali ya CCM ilitolewa na Mbunge Tundu Lissu akiituhumu serikali hiyo kwa kushindwa kuwaletea wananchi maendeleo.
Tangu siku hiyo wabunge wengi wa
upinzani wanaochangia hotuba ya Waziri Mkuu wamekuwa wakitumia lugha
hiyo huku Wabunge wa CCM wakijitutumua kuitetea kuwa haijachoka.
Mawerenewz.blogspot.com
ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na
HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI
pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>mawere_mtoka_mbali,SuScribe Youtube>>>MAWERE
No comments:
Post a Comment