05 May, 2015

Kingine kutoka Mahakamani Nigeria ni hii ishu ya deni analodaiwa D’Banj !!

Dbanj60
Hii ishu ilikuwa kama utani hivi, zikaanza stori kwamba D’Banj anadaiwa na jamaa mmoja Nigeria.. baadae tukasikia kwamba jamaa anayemdai ametishia kumshtaki.. leo hii story ina mwendelezo wake.
Henry Ojogho ambaye ni
makamu Mwenyekiti wa Broron Group and MindHub Technologies amesema anaidai Kampuni ya DKM Media ambayo inamilikiwa na D’Banj kiasi cha kama Naira Mil.60 ambazo ukiziweka kwenye hela yetu ni kama Tshs. Mil. 600 hivi.. kesi ilifika Mahakamani na kuanza kusikilizwa Lagos Nigeria, March 30 2015.
Siku hiyo ya kwanza kesi kusikilizwa Mahakamani wote wawili, yani D’Banj mwenyewe pamoja na Henry hawakuwepo Mahakamani.
Kesi ilisogezwa mbele na itasikilizwa tena Mahakamani siku mbili zijazo, yani May 7 2015.. D’Banj ni moja ya mastaa makubwa wenye mafanikio Africa ambaye anafanya kazi za kimuziki Marekani chini ya lebo ya G.O.O.D Music ambayo inamilikiwa na rapper Kanye West.
Kwenye list ya mastaa wa muziki wenye utajiri mkubwa zaidi Africa D’Banj yuko #3.. Hili deni ni kweli kashindwa kulipa au ni nini kinaendelea hapo??

No comments:

Post a Comment

Samsung kurejesha fedha kwa wanunuzi wa Note 7

KAMPUNI ya Vifaa vya Elektoriniki ya Samsung ya Afrika Mashariki (SEEA) itarejesha fedha kwa wateja wa simu za Note 7, ambao wataweza kuthib...