DAU LA KOCHA GORAN LAITOA JASHO SIMBA
Kupovic aliliambia gazeti la Mwananchi kwamba alizungumza na uongozi wa juu wa Simba kuhusu hatima yake kwenye club hiyo na walimweleza kwamba avute subira huku suala lake likifanyiwa kazi.
Baada ya kumaliza mkataba wake kocha Kupovic anataka mkataba mpya uwe na mshahara wa Dola
7,500(Sh 14.6 milion) kwa mwezi. Kocha huyo kutoka Serbia amekataa ofay a kulipwa Dola 5,000(Tsh 9.7 million). Habari kutoka gazeti la Mwananchi.
YUSUPH MACHO MUSSO ATOA ANGALIZO KWA NGASSA NA MSUVA
Baada ya Mrisho Ngassa kujulikana kwamba msimu ujao atacheza club ya Free State huko South Africa na Msuva akisubiri hatima yake, mchezaji wa zamani wa Yanga na Simba Yusuph Macho Musso ametoa angalizo kwa wachezaji hao wawili kuongeza umakini na juhudi au watasugua benchi.
“Licha ya ugumu wa ligi hiyo lakini imejaa ubaguzi wa hali ya juu, hadi mchezaji apewe nafasi inabidi aonyeshe uwezo wa hali ya juu”, alisema Musso akiongea na Mwananchi Michezo.
MBUYU TWITE AIGOMEA YANGA
Masilahi kidogo yameelezwa kukwamisha kusaini kwa mchezaji kiraka wa Yanga Mbuyu Twite. Habari za ndani zinasema Twite ameshindwa kufikia mwafaka wa Yanga iliyotaka kumpa fedha nusu za usajili zilizogomewa na mchezaji huyo ambae mkataba wake na Yanga umemalizika.
YANGA YATAMANI MAPESA YA MSUVA
Wakati uongozi wa klabu ya Yanga unakaa leo kumjadili winga wake Simon Msuva baada ya kutoroka kwenda kufanya majaribio bila ruhusa na timu ya Bidvest Wits, klabu hiyo ya Jangwani imeonyesha kutamani pesa za kumuuza Msuva.
Yanga wiki hii iliishia kunawa baada ya kutoka kappa katika uhamisho wa winga wake kipenzi Mrisho Ngassa aliyejiunga na Free State ambae alimaliza mkataba wake.Wana wajangwani wanahofia lisije kutokea kwa Msuva ambae amebakisha mwaka mmoja wa mkataba. Imeripotiwa na Nipashe Michezo.
NGASA ASEMA HAJAFIKA MWISHO SOUTH AFRICA
Kiungo mshambuliaji mpya wa timu ya Free State Stars ya South Africa Mrisho Ngassa amesema hajafika mwisho wa malengo yake ya kucheza soka la kulipwa baada ya kusajiliwa na club hiyo. Habari na Nipashe Michezo
STAND KUPATA UDHAMINI MNONO
Club ya Stand United iliyonusurika kushuka daraja inatarajia kupata udhamini mnono utakaowawezesha kufana maandalizi mazuri kwa michuano ya ligi kuu Tanzania bara.
Chanzo cha habari kimeliambia gazeti la Mtanzania kwamba tangu kumalizika kwa ligi Mei 9 klabu hiyo imeendelea na mazungumzo mazuri na mdhamini mpya.
NIYONZIMA : NAPUMZISHA AKILI
Kiungo wa timu ya Yanga Haruna Niyonzima amesema amejipa mapumziko ya wiki tatu kabla ya kuanza kufikiria kusaini mkataba mpya na klabu yoyote ya ligi kuu Tanzania Bara. Habari na gazeti la Mtanzania.
MANUEL PELLEGRINI ANAWEZA KUBAKI MANCHESTER CITY
Kocha Manuel Pellegrini mwenye miaka 61 anaweza akabakia msimu ujao na Manchester city baada ya review ilifanyika kwenye msimu 2014/2015. Limeandika gazeti la Guardian
MEMPHIS DEPAY ANATAKA KULIFUTA JINA LA CRISTIANO NDANI YA OLD TRAFFORD
Kijana mwenye miaka 21 ambae usajili wake umezungumziwa sana, Gazeti la Machester Evening News limeripoti kwamba ana nia ya kufanya makubwa Zaidi aliyoyafanya Cristiano kwenye club hiyo.
LIVERPOOL KUMSAINISHA MCHEZAJI WIKI HII
Winga wa Liverpool Jordon Ibe mwenye miaka 19 anatarajia kusaini mkataba mpya na Liverpool mapema wiki ijayo. Limeripoti gazeti la The Sun
CHELSEA YATOA OFA YA MIAKA MITANO
Klabu ya Chelsea imetoa ofay a miaka mitano kwa mchezaji timu ya taifa ya England under 21 Partick Bamford. Striker huyo ambae mwenye miaka 21 yupo Middlesbrough kwa mkopo na imeripotiwa anawavutia Everton,Aston Villa na Crystal Palace. Habari kutoka gazeti la Times
DANNY WELBECK ANATARAJIWA KURUDI KUTOKA KUWA MAJERUHI
Striker wa Arsenal Danny Welbeck mwenye miaka 24 anatarajiwa kurudi uwanjani jumapili hii kwenye mechi ya kugombania nafasi ya tatu. Daily Mail limeripoti.
NANI ANAJIPANGA KURUDI MANCHESTER UNITED
Winga wa Manchester united ambae alienda Sporting Lisbon kwa mkopo anatarajiwa kurudi Old Trafford msimu ujao. Habari zimetoka kwenye gazeti la Telegraph
No comments:
Post a Comment