MIPANGO ya usajili wa majira ya kiangazi wa Manchester United leo imetawala vichwa vya magazeti mengi barani ulaya .Gazeti la Times limeripoti
kuwa Man United wameweka rada zao zote kwa nyota wa Spurs, Harry Kane,
wakati magazeti mengine matatu yanasema
wanataka kumnunua GarBale.
wanataka kumnunua GarBale.
Magazeti ya The Express, The Mirror na The Star yanadai kuwa United wametenga paundi milioni 80 kumnunua Bale ambaye sasa haizuiliki kuondoka Santiago Barbebeu.
Hakuna wazo jipya juu ya United kumuwinda Bale kwani ilishawahi
kufanya hivyo hata kabla ya kutua Real Madrid, lakini The Mirror
limekuja na kona nyingine ya Stori likidai mashetani hao wekundu wako
tayari kuwauza Angel Di Maria na Robin van Persie ili kuongezea fedha za
kumsajili Bale.
Kumuuza Robin van Persie sio ishu kwasababu ya majeruhi yake ya
siku za karibuni, lakini kumuuza Angel Di Maria itakuwa stori kubwa
kwasababu amecheza mwaka mmoja tu tangu United walipovunja rekodi ya
usajili ya soka la Uingereza wakitumia karibia paundi milioni 60 kumleta
Old Trafford kutokea Real Madrid.
No comments:
Post a Comment