Mwamuzi mkubwa na mkongwe katika
mchezo wa ngumi Kenny Bayless ndiye atakayechezesha pambano la karne
linalosubiriwa kwa hamu kati ya Mmarekani Floyd Mayweather na Mfilipino
Manny Pacquiao litakalopigwa katika ukumbi wa MGM Grand Las Vegas tarehe
3 May 2015.
Mmarekani huyo mwenye umri wa
miaka 64 ,kwa kuchezesha pambano hilo atapokea kiasi cha dola z
kimarekani 25,000 (Paundi 16,600) ambazo ni sawa na Milioni 50 za
kitanzania.
Mapambano ambayo Kenny alishawahi
kuchezesha hapo awali ni Manny Pacquiao Vs Ricky Hatton,Oscar de la
hoyaVs Floyd Mayweather,Ricky Houtton Vs Paulie Malignaggi,Miguel Cotto
Vs Antonio Magarito,Manny Pacquiao Vs Miguel Cotto.
Kwa upande majaji ni Burt
Clements na Dave Morrett kutoka Las Vegas na jaji watatu ni Glenn
Feldmann ,ambao wote ni wazoefu katika kazi hiyo.
Majaji hao wote watatu watapokea kiasi cha dola za kimarekani 20,000 kutokana na kazi yao watayoifanya katika pambano hilo.
Kutokana mapato ya
viingilio,televisheni na vyanzo vingine,pambano hilo linataraji kuingiza
dola za kimarekani milioni 500 ambapo Floyd Mayweather atapokea dola za
kimarekani Milioni 150 huku Manny Pacquiao atapokea dola za
kimarekani milioni 99 bila ya kujali matokeo.
Mpaka sasa Pacquiao ameshinda
mapambano 57 kati ya 64 aliyowahi kupigana huku Mayweather akishuka
ulingoni mara 47 na kushinda mara zote
No comments:
Post a Comment