Usiku wa jana Uongozi wa klabu ya Liverpool ulitoa
zawadi kwa wachezaji wa timu hiyo ambao waliisaidia kwa kiasi kikubwa
katika msimu mzima wa ligi kuu, sherehe zilifanyika katika ukumbi wa Echo Arena . Nahodha anayeondoka Steven Gerrard ameshinda
tuzo ya
mafanikio ya muda mrefu ndani ya timu hiyo na anatarajia kuichezea timu hiyo kwa mara ya mwisho dhidi ya Stoke Jumapili kabla ya kuhamia LA Galaxy ya Marekani.
mafanikio ya muda mrefu ndani ya timu hiyo na anatarajia kuichezea timu hiyo kwa mara ya mwisho dhidi ya Stoke Jumapili kabla ya kuhamia LA Galaxy ya Marekani.
Mbali ya Gerrard pia Mshambuliaji kinda Raheem Sterling ametajwa
kama mchezaji bora chipukizi wa mwaka kwenye klabu hiyo licha ya baadhi
ya mashabiki wa klabu hiyo kumzomea kwa kitendo chake cha kytaka
kuihama timu hiyo huku Philippe Coutinho akitajwa kama mchezaji bora wa mwaka.Baada ya kupokea tuzo hiyo nahodha huyo aliwashukuru makocha wake pamoja
na wachezaji wenzake kwa ushirikiano waliouonyesha kwa kipindi chote
alichoichezea klabu hiyo.Kwa upande wa Manchester United pia walitoa tuzo kwa wachezaji wao ambapo kipa David de Gea anayetajwa kutaka kuhamia Real Madrid alishinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Manchester United na mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Hispania, Juan Mata ameshinda tuzo ya bao Bora la Msimu alilofunga katika mechi dhidi ya Liverpool.
No comments:
Post a Comment