TAARIFA mpya leo zinasema kocha
mkuu wa Simba aliyemaliza mkataba wake, Mserbia Goran Kopunovic
amekubali kurejea Dar es salaam kuendelea na kazi ya kuwanoa vijana wa
Msimbazi wenye uchu wa mafanikio kuelekea msimu mpya wa ligi kuu soka
Tanzania bara.
Tayari Simba kupitia kwa
mwenyekiti wa kamati ya usajili, Zacharia Hans Poppe walithibitisha
kuachana na Kopunovic kwasababu ya kutaka dau kubwa la usajili na
mashahara mrefu, hivyo kuanza harakati za kusaka kocha mpya.
Kopunovic alitakiwa kutoa jibu
kufikia Ijumaa ya wiki iliyopita kama atasaini mkataba mpya au la!,
lakini alishindwa kufanya hivyo.
Kopunovic alitaka dola za
Kimarekani 50,000 (sawa na Sh. Milioni 100) kama dau la kusaini Mkataba
na mshahara wa dola 8,000 (Sh. Milioni 16) kwa mwezi, kiasi ambacho
Simba walisema hawawezi kulipa.
Sasa Mserbia huyo amekubali
kushuka dau na atarejea nchini kuanzia juma lijalo kusaini Mkataba mpya
na mara moja kuanza maandalizi ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati, Kombe la Kagame.
Yuke kocha Mbelgiji Piet de
Mol aliyeripotiwa kuja kesho kuwania nafasi ya Kopunovic, atakuja kama
kawaida, lakini kutafuta kazi klabu nyingine.
No comments:
Post a Comment