Ligi kuu ya Soka Tanzania bara
leo imefikia ukingoni kwa kushuhudia michezo saba tofauti katika mikoa
sita tofauti, huku Mabingwa wapya wa ligi hiyo Dar es salaam Young
Africans wakijikuta wanapokea kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Ndanda FC,
Mtanange uliopigwa Mtwara katika
Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Uwanja wa Nangwanda Sijaona.
Kufatia ushindi huo Ndanda wanakuwa wamefikisha pointi 31 na kujiondoa kwenye mkasa wa kushuka daraja.
Uwanja wa Taifa Simba ilikuwa ikiminyana na JKT Ruvu ambapo matokeo yamepatikana kwa Simba kuibuka na Ushindi wa bao 2-1.
Chamazi jijini Dar es salaam
kunako uwanja wa Azam Complex, Wenyeji Azam FC wameweza kutoshana nguvu
kwa kugawana pointi na Mgambo JKT baada ya kutoa sare ya bila kufungana.
Shinyanga kwenye Uwanja wa CCM
Kambarage kulikuwa na mchezo kati ya Wenyeji Stand United ambao
waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting ambao wameshuka.
Mbeya City ambao walikuwa
wakiminyana na Polisi Morogoro kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya,
Walifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kufanikiwa kujikita katika
nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu hiyo ambayo imemalizika leo.Kufatia matokeo hayo ya leo Klabu za Polisi Morogoro pamoja na
Ruvu Shooting zinakuwa zimeporomoka daraja na kuzipisha timu nyingine
nne kushiriki ligi hiyo Msimu ujao. Mawerenewz.blogspot.com ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO,SIASA, na HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>Zawadi_mawere. Youtube>>>MAWERE TV.
TUPATIE MAONI YAKO>>>>
No comments:
Post a Comment