KOCHA mkuu wa Simba, Goran
Kopunovic bado hajafikia makubaliano na klabu yake kuhusu kusaini
mkataba mpya, lakini tayari ameshawaambia wachezaji wake kuwa yupo
katika mazungumzo na uongozi.
Kinachosababisha majaaliwa ya Kopunovic yasijulikane mpaka sasa ni dau kubwa analohitaji tofauti na bajeti ya Simba.
Ikumbukwe siku za karibuni
uongozi wa klabu hiyo kupitia kwa mwenyekiti wa kamati ya usajili,
Zacharia Hans Poppe ulikikiri kuwa klabu imeshuka kiuchumi kutokana na
mashabiki kutokwenda uwanjani.
Baadhi ya wachezaji wa Simba
wameeleza kuwa kama uongozi utashindwa kufikia makubaliano na kocha huyo
basi watakuwa wamepoteza bonge la kocha.
“Kopunovic ni bonge la kocha,
anajua kufundisha, ana msimamo, hababaishwi na viongozi kama ilivyokuwa
kwa Phiri (Patrick) ambaye alikuwa anapangiwa wachezaji na mazoezi ya
kuwapa wachezaji mechi ikikarabia.” Amefafanua mchezaji wa Simba ambaye
hakupenda jina lake kutajwa kwenye mtandao.
“Baada ya mechi ya mwisho na JKT
Ruvu, kocha alikaa na sisi wachezaji, akatueleza kuwa wapo kwenye
mazungumzo ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na akasema ikishindikana
basi tutaonana panapo majaaliwa”. Amesema mchezaji huyo na kuongeza:
“Hata haya mambo ya kishirikina Kopunovic hapendi kabisa, ujue Simba
kuna baadhi ya viongozi wanapenda sana mambo ya uchawi, eti hatuingii
vyumbani na kutozwa faini, mara mganga anatwambia tuchelewe kuingia
uwanjani, wachezaji wengine tuna imani zetu, yanatukera sana”.
Wakati huo huo, imefahamika kuwa
Simba inatarajiwa kutafuta makocha wengine kutoka nchi za Ufaransa,
Bulgaria, Senegal na Serbia.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe amekaririwa na Salehjembe
akisema mipango ya kuleta kocha mpya ipo ikiwa watashindwana rasmi na
Mserbia huyo na kuzitaja nchi hizo kuwa ndiyo zinazoweza kutoa kocha
wao.
“Ikiwa tutashindwana na
Kopunovic, kuna makocha kutoka nchi nyingi tu, wapo kutoka Ufaransa,
Senegal, Bulgaria na hata Serbia huko ambapo anatokea yeye,” alisema
Hans Poppe alipohojiwa na SalehJembe.
Kuhusu usajili mpya ikiwa ni siku
moja baada ya kutangaza wazi kutoendelea kuwa na beki Joseph Owino na
Dan Sserunkuma kiongozi huyo alisema nako pia kuna wachezaji kutoka nchi
kadhaa ambao wanajiandaa kuwaleta.
“Kuna wachezaji kutoka Ghana,
Burundi, Kenya, Rwanda na Nigeria, kote huko tumeshapata maombi na
mipango inafanyika kuja kufanya majaribio,” alisema.
Mawerenewz.blogspot.com
ndio mtandao wako wakipekee unaokupa habari za BURUDANI,MICHEZO, SIASA, na
HABARI MBALIMBALI ZA KIMATAIFA pamoja na KITAIFA Endelea kutembelea MTOKA MBALI
pia nifuate twitter>>>@mawere3, facebook>>>Mawere Mtoka Mbali, Instagram>>>Zawadi_mawere. SuScribe Youtube>>>MAWERE TV
No comments:
Post a Comment